Real Madrid, Barcelona Na Juventus Zajiandaa Kuzishtaki Mahakamani Team 9 Zilizojitoa Katika European Super League

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
Habari Wana Soka,

Taarifa za katika ulimwengu wa soka zinazohusiana na European Super League ilioandaliwa na team 12 kubwa barani ulaya zimechukua sura mpya.

Kutokana na taarifa hizo zinazoenea ni kwamba Real Madrid, Barcelona na Juventus zinajiandaa kuziburuza mahakamani Manchester United na Team 8 nyingine zilizojitoa katika mkataba wa kuanzisha European Super League.

● Team 9 katika 12 zilizokua zimeasisi mashindano ya European Super League zimetangaza nia ya kutaka kujitoa katika michuano hio, baada ya kupokelewa na wadau wa soka kwa kishindo kikubwa cha lawama.

● Real Madrid, Barcelona na Juventus zimekataa kutangaza nia ya kujitoa katika project hio.

● Kutokana na gazeti la New York Times kupitia kwa Daily Mail, team hizo 3 zilizokataa kujitoa katika project ya European Super League wameishatoa onyo kali kwa Manchester United na team zingine zilizotoa tamko la nia ya kujitoa katika project hio na kutarajia kulipa Mabillioni ya Euro kama penalty ya kutaka kujiondoa.

● Project ya European Super League ilipata misukosuko mwezi uliopita mara baada ya kutangazwa kuanzishwa kwake, kufikia hatua ya kutaka kufa ndani ya masaa 48 baada ya tamko hilo.

● Kutokana na barua ilioandikwa na Real Madrid, Barcelona na Juventus, waliotumiwa Manchester United na wenzao waliotaka kujitoa katika project hio, wameonywa kwamba ni kuvunja makubaliano ya kimkataba wa kuasisi league hio. Kutokana na mkataba kuwa na kipengele cha "KUTOKUJITOA LICHA YA KUTOKEA KWA JAMBO LOLOTE" kutokea katika makubaliano hayo ya kimkataba.

● Kutokana na barua hio ya onyo kali, muda wowote Manchester United na team zote zilizotoa tamko la nia ya kujitoa zitaburuzwa mahakamani kushurutishwa kuendelea na mkataba au kulipa penalty ya Mabillioni ya Euros.

Pitia thread.


- Shukrani New York Times, Daily Mail 07/05/2021.

 
Back
Top Bottom