RE: Kwa Watumiaji wa Antvirus kwenye Computer

RE: Kwa Watumiaji wa Antvirus kwenye Computer

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,700
Reaction score
4,126
Habari wana Jf!!

Nimeona tupate Elimu wote:


Mambo Muhimu Kuhusu Antivirus /Internet
Security
Watumiaji wengi haswa watumiaji wa
tarakishi
( computer/simu ) wanatumia vifaa vyao
hivyo na
kuingiza ( install ) programu za kulinda vifaa
hivyo dhidi ya virus na mashambulizi
mengine
kwa njia ya mtandao kama kifaa hicho
kimeunganishwa na mtandao .
JE ANTIVIRUS NI NINI
Antivirus ni programu inayowekwa katika
tarakishi ( computer/simu ) kwa nia ya
kulinda
tarakishi hiyo dhidi ya virus na ambao
wanaweza
kusambaa na kuhamishwa kwa njia nyingi tu .
INTERNET SECURITY NI NINI ?
Internet Security ina tabia na mambo mengi
kama antivirus lakini hii imeongezewa zaidi
nakwa wale wanaotumia mtandao ni virusi
kuwa
na Internet Security kuliko Antivirus .
Tofauti kubwa kati ya Internet Security na
Antivirus ni hiyo Firewall , lakini sio zote
ziko
hivyo .
AINA/MAKUNDI YA ANTIVIRUS
Kuna Makundi mengi ya antivirus
kutegemeana
na aina ambazo mtu anataka kwa ajili ya
shuguli
zake za kila siku .
Antivirus Huria /Bure (Free )
Hizi ni Antivirus ambazo unaweza kushusha
( download ) toka kwenye mtandao na
kuzitumia
kwa ajili ya ulinzi wa tarakishi yako lakini
huwa
zinakosa baadhi ya vitu au baadhi ya vitu
vimefungwa mfano wa Programu hizi ni AVG
2014 , AVAST 9.0 ,Kaspersky .
Utaona kwamba unatakiwa kusajili AVAST
ndani
ya siku 30 au itaacha kufanya kazi , AVG
haikulazimishi ila haina Firewall Kaspersky
nayo
inasiku 30 baada ya hapo itazima usipoweka
Leseni .
Trial/Demo ( Majaribio )
Antivirus hizi ni Bure kabisa na zinaweza
kupatikana kwenye tovuti kadhaa lakini
matatizo
yake ni kwamba zenyewe ni za muda fulani
baada ya muda huo zinajifunga hazitoweza
kufanya kazi mpaka ununue leseni yake kwa
njia
ya mtandao kampuni zinazotoa antivirus za
majaribio ni kama Symantec yenye Norton
Antivirus na Kaspersky .
Full Version /Licensed /Za Kununua
Mara nyingi mtaani watu wanaita za kununua
kwa sababu unakuwa unapata kila kitu na
kama
unahitaji Keys au Leseni yake unaweza
kuiona
imeandikwa au iko ndani ya CD yenye
Programu
hiyo au kama umenunua kwa njia ya mtandao
basi utatumiwa kila kitu kwenye Anuani ya
Barua
pepe yako na maelezo ya kutosha .
Cha muhimu kujua ni kwamba ubora wa
antivirus
hautegemei na bei ya antivirus uliyonunua
au
aina ya antivirus uliyonunua mara nyingi
inategemea hata mazingira unayofanyia kazi
na
aina za kazi unazofanya na mambo mengi
zaidi .
Ni vizuri ukanunua antivirus na kuwa na
leseni
yake ili siku nyingine uweze kutumia leseni
hiyo
kama limetokea tatizo kwenye tarakishi yako
na
kuamua kufuta vitu .
VIRUS WANASAMBAA KWA NJIA GANI
Kuna njia kuu 2 ambazo zinaweza kusambaza
Virus
Moja ni kwa kutumia vichomekwa kama
Flashdisk , hii mara nyingi inatokea pale mtu
anapoingiza flashdisk yake kwenye tarakishi
iliyoadhirika na virus .
Mbili ni kwa njia ya mtandao hii inatokea
pale
mtu anaposhusha ( download) viru kutoka
kwenye mtandao kama ni programu ambayo
inaweza kuwa na virus ( hii inategemeana na
chanzo cha programu hiyo ) au faili ambalo
anaweza kuwa ametumiwa na mtu .
Njia nyingine zilizobaki hazitumiwi sana na
wahalifu na kama zikitumiwa basi huwa na
malengo fulani haswa yanayohusiana na
ujasusi
na aina nyingine za uharamia kwa njia ya
mtandao .
MAISHA YA ANTIVIRUS
Maisha ya Antivirus yanaanza pale
unapoingiza
kwenye tarakishi yao au vifaa vingine vya
mawasiliano kama simu ya mkono .
Maisha ya antivirus mara nyingi ni muda wa
mwaka mmoja lakini inategemeana na leseni
uliyonunua kwenye bidhaa husika wengine
wanatoa hata miaka 2 kwahiyo ni kuanzia siku
uliyoweka mpaka mwaka siku zaidi ya 300
ziishe .
Jambo muhimu kuliko zote kujua ni kwamba
pale unapoingiza antivirus kwenye tarakishi
yako
inakuwa tayari imeshapitwa na wakati
( outdated ) na nguvu yake inakuwa
imepungua
kwa kiasi kikubwa sana unatakiwa uweke
updates ili iweze kwenda na wakati na kuwa
imara .
Watu wengi wanapenda kuweka antivirus
kwenye
tarakishi zao na programu nyingine bila
kuziboresha zaidi ( kufanya updates )
matokeo
yake ni kwa programu hizo au antivirus hizo
kufanya kazi chini ya kiwango na kushindwa
kupambana na virus na matishio mengine
yaliyopo kwenye ulimwengu wa tarakishi
haswa
kwa njia ya mtandao .
MWISHO WA ANTIVIRUS .
Mwisho wake ni pale mtu anapochoka
kutumia
bidhaa hiyo na kuamua kutumia bidhaa
nyingine
anaamua kuiondoa kwenye tarakishi yake ,
kama
imefikia hivyo unaweza kutumia njia ya ADD/
REMOVE PROGRAMES au UNINSTALL au
unaweza
kutafuta programu maalumu ya kuondolea
programu hiyo .
Kwa sasa kampuni nyingi zinazotengeneza
antivirus zina programu maalumu kwa ajili ya
kuondolea bidhaa zao kwenye tarakishi
unaweza
kupata bure programu hizo .
Somo langu linaishia hapa kwa leo , ukitaka
habari na maarifa zaidi unaweza kutafuta kwa
njia ya mtandao na kusoma zaidi , hichi
nilichoandika ni kwa ajili ya kufundisha tu ,
elimu
zaidi unaweza kuipata kwa njia ya mtandao
na
vitabu au makala mbalimbali.


SOURCE:https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=687921624577563&id=100000791940063&refid=7&_ft_=qid.6009900747887428545%3Amf_story_key.-8504590228395429280&__tn__=%2As
 
Threads ina makosa mengi !
Ntarudi baadae !
 
Back
Top Bottom