Re: CIGAR imekuwa sumu kwa mahusiano

Re: CIGAR imekuwa sumu kwa mahusiano

Getruda

Member
Joined
May 10, 2012
Posts
16
Reaction score
4
Salamu kwenu MMU,
Ni binti mtanzania, ninavuta sigara tangia nilipomaliza tu high school hadi leo nimemaliza chuo nimeajiriwa mahali. Kazi yangu inaniweka busy sana kiasi napatikana mjini kwa nadra.

Ni mekuwa na stlye yangu tofauti ya maisha kwamba naishi nitakavyo no matter what my family, friends na community watasema au wanafanya. Familia yangu ni yenye dini sana na yenye maadili (kama walivyojiwekea na ilivyozoeleka na kukubalika miongoni mwa watanzania. Ninasema hivi kwa sababu maadili ni located and subjective. Unayoyaita maadili Tanzania sehemu nyingine si maadili ni kitu kingine. Hivyo inategemeana na wewe binafsi umeamua uishi vipi). NINAOMBA TUSIJADILI HILI KWENYE POST HII KWANI NI KAMA BACKGROUND INFO TU. Kwa msingi huu wananiona kama deviant kwa kuamua kuwa mvutaji bila kificho, kuishi party life (lakini nasave kwa ajili ya badae sio kwamba nimejisahau) ila mimi nimejikubali na nimeamua kuishi maisha yangu niliyojiamulia na kujiwekea.

Swala la sigara limekuwa ni tatizo kwa familia yangu, ndugu na hata mahusiano. Mimi kuacha imekuwa ngumu. Mwanaume wangu alinikuta navuta cigar na alidai alinipenda kwa sababu ya utofauti wangu na kusimamia kile nikiaminicho lakini hata sijui imeanzia wapi anadai hawezi kuoa mwanamke mvutaji (lakini sivuti bangi, ni SM na zinginezo tu. Hata sigara kali sivuti). Sasa ninajiuliza huyu hakuniona mwanzoni kwamba navuta? je niendeleze msimamo wangu au niache kwa ajili yake? kama ni kuacha nawezaje kuacha kwani nimeizoea sigara na kuipenda kama vile chakula maishani mwangu? Kwa siku siwezi hata kuhesabu navuta pakti ngapi tena ukizingatia nina kampani ya mvutaji mwenzangu ambae ni boss wangu kikazi 30/7. Hili limekuwa ni swala gumu sana maishani mwangu na ninaona kama nitampoteza huyu mshikaji (boyfriend).

Ninaomba mnishauri kwasababu niko njia panda. Kwa wenye matusi au kuhukumu hapa sio mahala penu kwani familia ilishanihukumu tayari amebaki Mungu wangu tu kunihukumu.

Asanteni na karibuni mnipe ushauri akili imestak.
 
Hayani mahubiri ya familia daily. Ila sawa niambie njia za kuiacha?
si unaacha kuvuta tu mwenyewe kwani kuna mtu anakushkia ukivuta.mabadiliko yoyote yanaanzia kwako mwenyewe
 
Pamoja na alikuona unavuta cigar lakini alikupenda kwa dhana kwamba kama mapenzi yenu yatashamiri angeweza kukubadili ili uachane na uvutaji wako. Una bahati huyo ameweza kuvumilia uvutaji wako wengine baada ya kujua kama wewe ni mvutaji hata nafasi ya kuwa mupenzi wao wasingekupa. Katika mapenzi kuna baadhi ya tabia zinakubalika na nyingine hazikubaliki na hii inatofautiana kati ya mtu na mtu. Kama unampenda na hutaki kumpoteza basi ni lazima uachane na uvutaji vinginevyo atasepa kivyake vyake.
 
Nikiwa na my boss (mtasha) huwa navuta sana cigar ila kitaa nakuwa na sigareti

Hapo ndo unapoharibu dada! Una mix cigar na cigarette? Mbna unageuka jiko la kuni?

mbaya zaid unavuta SM na vip una2mia vinywaji barid?
nakushauri kuvuta ni starehe yako anaekereka ni matatzo yake binafsi ila cha muhimu kuwa na brand yako ya sigara si kuvuta tu kila sigar ucje ukaharibu mapafu kwa kugeuka jiko la kuni huchagui.

Kila sigara au cigar iko na chemical composition tofauti na imapact tofauti kuacha nicotin ambayo ndo iko na pasee kubwa kwenye fegi.
 
ana misimamo yake eti anayoisimamia eti! sipendi mtu mwenye kauli hizi.
Pamoja na alikuona unavuta cigar lakini alikupenda kwa dhana kwamba kama mapenzi yenu yatashamiri angeweza kukubadili ili uachane na uvutaji wako. Una bahati huyo ameweza kuvumilia uvutaji wako wengine baada ya kujua kama wewe ni mvutaji hata nafasi ya kuwa mupenzi wao wasingekupa. Katika mapenzi kuna baadhi ya tabia zinakubalika na nyingine hazikubaliki na hii inatofautiana kati ya mtu na mtu. Kama unampenda ha hutaki kumpoteza basi ni lazima uachane na uvutaji vinginevyo atasepa kivyake vyake.
 
Kama unathamini kuvuta kuliko hao wanaotaka uache, endelea kuvuta.

La,

Kama unawathamini hao wasiopenda uvute kuliko unavyothamini kuvuta, acha kuvuta.

Simple like that.
 
Ndio hapo sasa Smile!!! afanye modification kwenye misimamo yake isiyo na tija au akubali kumkosa mchuchu, kupanga ni kuchagua.

ana misimamo yake eti anayoisimamia eti! sipendi mtu mwenye kauli hizi.
 
Last edited by a moderator:
Dutch master

The boss hizi ninatumia niliwa na boss. mie hela zote hizo nitatoa wapi.. ila muhimu utoe ushauri kuliko kuniweka kama niko polisi kwa maswali mengi.


Ushauri best ni uvute ukiwa alone
wakiwepo hao usivute
 
Back
Top Bottom