Mgibeon
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 11,257
- 21,286
Wakuu kufuatia namna ya ajabu kabisa ya hawa wakuu wa mikoa na wilaya wanavyotimiza majukumu awamu hii, naona bora tubadilishe utaratibu wa kuwapata hawa ndugu zetu.
Ukiangalia matatizo mengi yanayojitokeza yanayoleta malalamiko kwa raia ni hawa ndugu zetu, ukijiuliza kwanini wanapower kiasi hicho jibu linakuja kua kwakua wameteuliwa na Rais. Hivi ni kweli mtu aliepewa madaraka na mtu mmoja ni bora kuliko yule aliechaguliwa na raia wake?
Tunaomba Wabunge wapeleke jambo hili Bungeni lifanyiwe mabadiliko, Wakuu wa mikoa na Wilaya nao wafanyiwe utaratibu wa kuwapata kama wanavyopatikana wabunge.
Laiti kama hawa Wakuu wangekua wamechaguliwa kwa kura haya matatizo yasingekuwepo. Tunataka Uhuru wa maoni na kuchagua yule tunaemtaka. Rais abaki na mamlaka mengine yanamtosha sana.