johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,285
- 142,471
Mkuu wa mkoa wa Tanga mh Shigela amesema watu wawili walioripotiwa Zanzibar kuwa ni wagonjwa wa Corona waliotokea Tanga huenda maambukizi hayo waliyapata ndani ya boti au bandarini Unguja.
Shigela amesema wamezitembelea familia za wagonjwa hao jijini Tanga na kuzikuta zikiwa buheri wa afya hata hivyo wameziweka katika karantini kwa mujibu wa taratibu za nchi.
Naye mkuu wa wilaya ya Pangani amesema katika boti waliyopanda hao wagonjwa kulikuwa na abiria 6 na mmojawapo ni raia wa Ujerumani ambaye wanamfuatilia.
Source Eatv habari!