RC na DC ni watumishi wa umma?

RC na DC ni watumishi wa umma?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2017
Posts
529
Reaction score
905
TUMALIZE UBISHI

TANGAZO;
"Serikali yetu inaanza ukaguzi wa vyeti vya Watumishi wa Umma mara moja." = JPM

HOTUBA;
"Uhakiki huu wa vyeti haukuhusisha VIONGOZI WA KISIASA ambao ni Mawaziri, Wabunge, Madiwani, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya" = Waziri Angela Kairuki.

SHERIA;
Sheria mama inayosimamia watumishi wote ni Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002. Kifungu cha 3 kinaeleza maana ya mtumishi wa umma “public servant”. Kinasema hivi, “Kwa muktadha wa sheria hii, mtumishi wa umma ni mtu anayeshikilia madaraka au kukaimu madaraka katika ofisi ya utumishi wa umma”.

Sheria hiyo imekwenda mbali zaidi katika kifungu hicho hicho cha 3 na kueleza maana ya “Ofisi ya Utumishi wa Umma” (public service office). Sheria inasema, “kwa muktadha wa sheria hii, Ofisi ya Utumishi wa Umma inamaanisha;

(a)Ofisi inayogharamiwa na umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ina jukumu la kutengeneza sera za serikali na kutoa huduma za kijamii.

(b) ofisi yoyote ambayo itakuwa imeazimiwa/imetangazwa na sheria au iliyoko chini ya sheria yoyote kwamba ofisi hiyo itakuwa ofisi ya umma.

KWA HIYO;
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ni Watumishi wa Umma 100% na hata mamlaka inayowateua inawateua katika misingi hiyo hiyo ya utumishi. Kwa hiyo kama tuliutangazia umma kuwa "tunakagua vyeti vya WATUMISHI WA UMMA" then sheria iko wazi kuwa RCs na DCs ni watumishi wa umma.

JE RC's na DC's NI WANASIASA?
1. Nimemsikia Waziri, dada yangu Angela, akieleza kuwa Uhakiki wa Vyeti haukufanyika kwa viongozi wote wa kisiasa, anawataja "Mawaziri, Wabunge, Ma RC, Ma DC na Madiwani.

Kuwaingiza RC's na DC's kwenye kundi la wanasiasa ni upotoshaji wa kiwango cha juu kabisa. Wakuu wa Mikoa (RC's) na Wakuu wa Wilaya (DC's) siyo viongozi wa kisiasa na hawaongozi Ofisi za Kisiasa. Mkuu wa Mkoa ni msimamizi wa juu za mkoa mzima (a supervisor), huyu si mwanasiasa na haijawahi kuwa hivyo.

Na ndiyo maana mara kadhaa mmewasikia ma RC na ma DC waking'aka kuwa "mimi siyo mwanasiasa" ila ni wasimamizi wakuu wa shughuli za serikali kwenye mikoa yao.

2. Kimkakati, CCM ilianzisha mfumo huu wa nafasi za RC's na DC's ili kuunganisha shughuli za chama na serikali nchi nzima. Yaani, ni mfumo ambao usingelikuwepo (let us say tungelikuwa na Ma RC na Ma DC wanaochaguliwa au kuteuliwa bila upendeleo au na wananchi wenyewe), CCM ingelikosa kabisa watu wenye mamlaka ngazi za mikoa na wilaya ambao hupaswa kutumika kutetea maslahi ya CCM dhidi ya maslahi ya taifa/wananchi ili kulinda madaraka yasiende nje ya CCM asilani abadani!

Kwa hiyo, hoja ya Angela Kairuki (Waziri) kwamba ma DC na ma RC ni wanasiasa inasemwa ili "ku-qualify" aibu na soni ambazo zimekuwa zikifanyika kwa kuwatumikisha ma RC na ma DC kwa maslahi ya CCM ikiwemo kuingilia na kuhujumu chaguzi, kuhujumu mamlaka ya vyombo vya dola ambavyo vinapaswa kufanya kazi zake proffessionally n.k.

3. Na tena, hoja ya Angela Kairuki inajaribu kuwazoesha wananchi jambo lisilopaswa kuwapo, la kudhania na kuona ni sawa tu ma RC na ma DC wakiwa wanasiasa. Hapa duniani ukitaka jambo lako liende, mzoeshe unayemuongoza kuona "umasikini ndiyo utajiri" na kuwa "umasikini haukwepeki".

4. Dhana hii nayoijadili hapa ni sawa sawa na ile ya JPM kuteua na kujaza makada wa CCM kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Halmashauri na Manispaa bila kujali kule zile ni za utendaji wa ndani mno na kwamba zinapaswa kukabidhiwa kwa watumishi wa umma wenye uzoefu na uwezo mkubwa.

Kimkakati, uamuzi ule wa JPM ulifanywa kama chambo cha kuandaa hujuma na kupata wana CCM wa kutosha kwenye ngazi za chini ambao ni rahisi kuwapigia simu moja tu "huyo mgombea wa upinzani asitangazwe hata kama atashinda" na wakatekeleza!

Haya mambo ni makubwa kushinda tudhaniavyo, lakini kimantiki, kisheria, kiweledi, kikatiba n.k. RC's na DC's siyo sehemu ya wanasiasa, it only happens in the CCM regime.

Nisameheni kama nimezungumza kifalsafa sana.

Tujifunze kutafakari na kujadili.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J
 
Aendelee tu kuchambua

Hakuyasaka haya hadi now
Kweli watu mmeshushuka ha ha haaaa

Mbona yeye ubunge aliotaka amewekwa pembeni hata kufungua mdomo nusu kuhoji mabosi wake kashindwa ha ha haaaa

Serikali imetamka anayepinga aende mahakamani.

Tena upinzani ndio mnapapenda mkifikiri mnavutia watu kujiunga na chama chenu....jaribuni mengine.
 
Hapa umejadili nini? Wakati mwingine ni vizuri kuficha kilichojaza kichwa chako, hasa ikiwa huna hakika kichwan mna nn.
Mtoa mada kaeleza vizuri tena kwa kiricite vifungu vya sheria kuwa dc, rc ni viongozi wa umma. Sasa wewe tuambie kwa nini sio watumishi wa umma na sio kuandika nonsense hata kwenye issue sensitive kama hizi.
 
Mind your own business.

Forum hii, andika yako niandike yangu.

Mtanyooka tu, serikali imesema full stop.
 
Heri wenye moyo safi maana wataurithi ufalme wa mbingu
 
Wakurugenzi wa halmshauri za wilaya, miji, manispaa na majiji wataitwa viongozi wa kisiasa.
 
Heri wenye moyo safi maana wataurithi ufalme wa mbingu
Kweli Mkuu, Maandiko matakatifu pia yanasema katika Mathayo 5 mstari wa 6 kuwa, heri wenye kiu na njaa ya HAKI, maana hao watashibishwa.
 
TUMALIZE UBISHI

TANGAZO;
"Serikali yetu inaanza ukaguzi wa vyeti vya Watumishi wa Umma mara moja." = JPM

HOTUBA;
"Uhakiki huu wa vyeti haukuhusisha VIONGOZI WA KISIASA ambao ni Mawaziri, Wabunge, Madiwani, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya" = Waziri Angela Kairuki.

SHERIA;
Sheria mama inayosimamia watumishi wote ni Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002. Kifungu cha 3 kinaeleza maana ya mtumishi wa umma “public servant”. Kinasema hivi, “Kwa muktadha wa sheria hii, mtumishi wa umma ni mtu anayeshikilia madaraka au kukaimu madaraka katika ofisi ya utumishi wa umma”.

Sheria hiyo imekwenda mbali zaidi katika kifungu hicho hicho cha 3 na kueleza maana ya “Ofisi ya Utumishi wa Umma” (public service office). Sheria inasema, “kwa muktadha wa sheria hii, Ofisi ya Utumishi wa Umma inamaanisha;

(a)Ofisi inayogharamiwa na umma katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ina jukumu la kutengeneza sera za serikali na kutoa huduma za kijamii.

(b) ofisi yoyote ambayo itakuwa imeazimiwa/imetangazwa na sheria au iliyoko chini ya sheria yoyote kwamba ofisi hiyo itakuwa ofisi ya umma.

KWA HIYO;
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya ni Watumishi wa Umma 100% na hata mamlaka inayowateua inawateua katika misingi hiyo hiyo ya utumishi. Kwa hiyo kama tuliutangazia umma kuwa "tunakagua vyeti vya WATUMISHI WA UMMA" then sheria iko wazi kuwa RCs na DCs ni watumishi wa umma.

JE RC's na DC's NI WANASIASA?
1. Nimemsikia Waziri, dada yangu Angela, akieleza kuwa Uhakiki wa Vyeti haukufanyika kwa viongozi wote wa kisiasa, anawataja "Mawaziri, Wabunge, Ma RC, Ma DC na Madiwani.

Kuwaingiza RC's na DC's kwenye kundi la wanasiasa ni upotoshaji wa kiwango cha juu kabisa. Wakuu wa Mikoa (RC's) na Wakuu wa Wilaya (DC's) siyo viongozi wa kisiasa na hawaongozi Ofisi za Kisiasa. Mkuu wa Mkoa ni msimamizi wa juu za mkoa mzima (a supervisor), huyu si mwanasiasa na haijawahi kuwa hivyo.

Na ndiyo maana mara kadhaa mmewasikia ma RC na ma DC waking'aka kuwa "mimi siyo mwanasiasa" ila ni wasimamizi wakuu wa shughuli za serikali kwenye mikoa yao.

2. Kimkakati, CCM ilianzisha mfumo huu wa nafasi za RC's na DC's ili kuunganisha shughuli za chama na serikali nchi nzima. Yaani, ni mfumo ambao usingelikuwepo (let us say tungelikuwa na Ma RC na Ma DC wanaochaguliwa au kuteuliwa bila upendeleo au na wananchi wenyewe), CCM ingelikosa kabisa watu wenye mamlaka ngazi za mikoa na wilaya ambao hupaswa kutumika kutetea maslahi ya CCM dhidi ya maslahi ya taifa/wananchi ili kulinda madaraka yasiende nje ya CCM asilani abadani!

Kwa hiyo, hoja ya Angela Kairuki (Waziri) kwamba ma DC na ma RC ni wanasiasa inasemwa ili "ku-qualify" aibu na soni ambazo zimekuwa zikifanyika kwa kuwatumikisha ma RC na ma DC kwa maslahi ya CCM ikiwemo kuingilia na kuhujumu chaguzi, kuhujumu mamlaka ya vyombo vya dola ambavyo vinapaswa kufanya kazi zake proffessionally n.k.

3. Na tena, hoja ya Angela Kairuki inajaribu kuwazoesha wananchi jambo lisilopaswa kuwapo, la kudhania na kuona ni sawa tu ma RC na ma DC wakiwa wanasiasa. Hapa duniani ukitaka jambo lako liende, mzoeshe unayemuongoza kuona "umasikini ndiyo utajiri" na kuwa "umasikini haukwepeki".

4. Dhana hii nayoijadili hapa ni sawa sawa na ile ya JPM kuteua na kujaza makada wa CCM kwenye nafasi ya Ukurugenzi wa Halmashauri na Manispaa bila kujali kule zile ni za utendaji wa ndani mno na kwamba zinapaswa kukabidhiwa kwa watumishi wa umma wenye uzoefu na uwezo mkubwa.

Kimkakati, uamuzi ule wa JPM ulifanywa kama chambo cha kuandaa hujuma na kupata wana CCM wa kutosha kwenye ngazi za chini ambao ni rahisi kuwapigia simu moja tu "huyo mgombea wa upinzani asitangazwe hata kama atashinda" na wakatekeleza!

Haya mambo ni makubwa kushinda tudhaniavyo, lakini kimantiki, kisheria, kiweledi, kikatiba n.k. RC's na DC's siyo sehemu ya wanasiasa, it only happens in the CCM regime.

Nisameheni kama nimezungumza kifalsafa sana.

Tujifunze kutafakari na kujadili.

[HASHTAG]#Mtatiro[/HASHTAG] J
Mtatiro utaandika mengi sana lakini yasilete maana hasa ambayo hili zoezi lilikuwa linafanya.

Hao unaowataka wahakikiwe nafasi zao hazisomewi,hazina kozi yoyote,hazina cheti chochote!

Sasa unataka wahakikiwe nini? Sifa yao ni moja tu uwe unamjua kusoma na kuandika basi haijalishi umesoma mpaka level gani ya elimu.

Hakuna mahali utakapo lazimimisha jambo liwe kwa jinsi unavyotaka wewe.

Hata kama wanatumikia umma na hizo Ofisi kuziita za umma hao kuwaita watumishi wa umma lakini root yao ni kutokea mlango wa siasa ambao sifa zao ndiyo kama nilivyozitaja hapo juu.

Shida yako kubwa ni maneno ya mitaani yalizagaa tu kuhusu elimu ya Paul Makonda aliyemaliza Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi basi hakuna lingine.

Zoezi hili halimuhusu!!
 
Naomba kuuriza rc or dc ni wanasiasa au ni watumishi wa umma?

Na kama ni watumishi wa umma sheria ya utumishi wa umma inasemaje hapo. Ni kifungu kipi kinamruhusu mtumishi kuonyesha hadharani mapenzi yake kwa chama cha siasa?
 
Suluhisho ni katiba mpya ,,kwa ccm kupindisha sheria ruksa
 
Mkuu ni haki yake kikatiba kuhama chama Lakini kuweka mahaba ya chama wazwaz hapo hata mm napata mashaka juu ya hili Mfano hapo Dodoma Leo kuna tamasha au sijui n tukionana la UZALENDO Lakini Badala yake limekuwa tukio LA chama la watu kwenda kujitambulisha kuhamia CCM Nadhan nchi hii uzalendo ni kuwa CCM na waliopo nje ya ccm maana yake Si WAZALENDO
 
Let's be realistic jama!hakuna dc,rc,ps,dvc,vc judge,rpc,rco,tiss na mfano wao....ambaye siyo kada bana!aah kwanini tuishi ndotoni!!!
 
Yes Ni realistic lakini ndio Sheria inaruhusu hivyo mkuu?

Nini kifanyike then?
 
Sheria inasema hivi.At such a position in public service,utawajibika kwa sera za chama kilichoko madarakani kwa wakati huo. Utazifafanua,utazinadi na utazitenda, sasa yanini kujidanganya? Kama nakosea nisahihishe mkuu,elimu yangu ni ya hapa na pale.
 
Back
Top Bottom