RC Mwanza atoa miezi miwili kwa watendaji wa mitaa,wilaya kumaliza tatizo la uhaba wa madawati

mgeni wenu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
3,664
1,730
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ametoa muda wa miezi miwili kuanzia sasa hadi juni 30 mwaka huu, kwa watendaji wa ngazi ya mitaa hadi wilaya mkoani humo, kuhakikisha wanamaliza tatizo la uhaba wa madawati katika shule mbalimbali za msingi na mtendaji yeyote atakayeshindwa kutekeleza agizo hilo atakuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe.
 
Duh kwaio watendaji watoe fedha zao mfukoni watengeneze madawati
 
Wamalize kero za madawati kwa pesa ipi? Sasa pesa yote itatumika kwenye madawati tu huduma zingine zisimame?
 
Bila mchanganuo wa kueleza pesa zitatoka wapi hapo ni sawa na kumwambia mkeo nikirudi nyumbani nikute umenipikia pilau na nyama ya kuku wakati huo ukijua kabisa haujaacha hata senti tano. Sasa hao watendaji watatoa pesa zao mfukoni?
 
Hivi kwanini hawa wakuu wa mikoa wamekuwa majeuri sana.

Tanzania toka ipate Uhuru mwanafunzi walikua wanakaa chini yeye Leo hii aje awape madiwani wiki mbili wawe wamemaliza hilo tatizo.

Kwa misingi ipi Na wakati huo yeye anaonge tu hamna jitihada zozote anazo zifanya.
Kuhakikisha hayo madawati yanapatikana.
 
Sijamuelewa kabisa huyo RC, sasa watapata wapi pesa ndani ya week 2 ikiwa serikali imeshindwa ndani miaka 54 ya uhuru? Ni sawa na Makonda anawataka watendaji wa mitaa wa Dar kufanya sensa ya nyumba zote kwa gharama zao ila hakumbuki kuwa wale hawana posho wala mishahara anawatuhumu kuwa kazi zao si kutoa barua za dhamana na kufungua account banks! Kazi ipo miaka 5 hii!....
 
Mzee wa harambee yuko wapi? Amekaa kimya sana kwani hangetuletea rafiki zake wale tungemaliza tatizo la madawati Tanzania nzima.
 
Awamu hii ukiwa mbele ya waandishi inabidi useme chochote tu cha kufurahisha mamlaka ya uteuzi, hata kama hakitekelezeki!
 
Hadi raha ni matamko kwa kwenda mbele sasa hakuna mipango hakuna takwimu hakuna maelezo ya kitaalam na kitaaluma hakuna bajeti ni kutamka tu iwe hata kama ni kwa miujiza
 
Back
Top Bottom