JAMHURI
JF-Expert Member
- Dec 15, 2010
- 449
- 60
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amesema, ataendelea kumsifu kiongozi atakayefanya kazi hata kama wengine watachukia.
Mnyeti ameyasema hayo wakati wa ukaguzi wa miradi ya ujenzi alioufanya Kiteto.
Miradi mingi ya ujenzi Kiteto iko kwenye kiwango kinachostahili hivyo nitaendelea kumsifu anayeisimamia kikamilifu
Kiteto ya leo sio ile tuliyoikuta miaka miwili iliyopita, kuna mabadiliko mengi ambayo yanafanywa na hawa viongozi.
Wengine sasa wanatakiwa kuja kujifunzi, kuna mabweni ya wanafunzi Sekondari ya Kiteto yanaridhisha
Maeneo mengine kuna tofauti ya mil 20 na ni ukubwa kama huu kwanini msimamizi asisifiwe?alihoji
Tumim Kambona ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kiteto, pamoja na mambo mengine amejizolea sifa kwa kipindi kifupi cha miaka miwili katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Pamoja na mambo mengine Kambona anasimamia mradi wa ujenzi wa jengo la Serikali la bil 4.3, uboreshaji wa kituo cha Afya Sunya mil 400, mabweni mawili ya sekondari ya Engusero na madarasa katika shule mbalimbaki za msingi na Sekondari mbali na miradi mingine.