Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,260
Nimesoma kwa masikitiko habari katika gazeti la Mwananchi la tarene 12/06/2016 juu ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya kukifunga chuo cha Meya Polytechnic kwa madai ya kukiuka taratibu za uendeshaji na hivyo kusababisha taharuki na usumbufu mkubwa kwa wanafunzi zaidi ya 2000 na wafanyakazi.
Mimi naona alichofanya ni kama walichofanyiwa wale wanafunzi wa UDOM. Ingekuwa ni vema angewapa muda wamiliki wa chuo kutimiza masharti na taratibu badala ya kukifunga na hivyo kuwakosesha masomo wanafunzi zaidi 2000 na kupoteza ajira za watu. Unapofunga chuo ghafla vile na kukiwa na watu zaidi ya 2000 ni hatari sana kwani inawaathiri wanafunzi na wazazi kisaikoloji na kiuchumi. Amesema eti chuo kirudishe ada za wanafunzi. Hii inashangaza kwani ni kama vile anafikiri ada yote iliyokusanywa imewekwa kwenye boksi hivyo ni ya kuchota tu na kurudisha. Hilo haliwezekani kwani chuo kilikuwa kinaendelea hivyo ni dhahiri sehemu kubwa ya pesa imetumika kuendesha chuo ikiwa ni pamoja na mishahara ya wafanyakazi, vifaa, vyakula, umeme, maji, mafuta na matumizi mengine mengi ya kuendesha chuo sasa chuo kitarudisha kupita chanzo kipi cha pesa?
Kwa maoni yangu ingekuwa vema kabisha ange kaa na uongozi wa chuo na kuwapa muda maalumu wa kurekebisha kasoro zote ikiwa ni pamoja na usajili kwani hicho chuo kimekuwepo muda mrefu kama ni makosa basi yanahusu pia hata serikali kuruhusu hali hiyo kuwepo. Viongozi wa sasa wanaona ni sifa kufanya maamuzi ya nguvu bila kujali athari ambazo raia wanapata. Wakati wa utawala wa JK alikuwa akisema kuwa pamoja na kutaka sheria ifuatwe lakini inatakiwa kutumia busara kubwa sana kama kiongozi unapochukua maamuzi ya kutaka kusimamia sheria iliyokwisha vunjwa kwani unaweza kujikuta wewe ndiyo unasababisha madhara mkubwa zaidi kuliko wao waliovunja kwanza sheria. Maamuzi ya pupa kwakeli ni hatari sana hasa katika nyakati hizi ambazo kila kiongozi anataka aonekane anafanya kazi
"Wanafunzi wahaha Mbeya baada ya chuo kufungwa
Wanafunzi walipatwa taharuki huku baadhi yao wakizimia baada ya agizo la Makallla la kukifunga chuo hicho ambacho awali kilikuwa kikijulikana kama Ihemi Polytechnic College
Mbeya. Takribani wanafunzi 2,000 wako njiapanda baada ya Chuo cha Mbeya Polytechnic kufungwa kwa madai ya kukiuka taratibu za uendeshaji.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amechukua hatua ya kukifunga chuo hicho jana kwa madai kuwa kinatoa mafunzo ya kilimo, huku kikiwa hakijapewa kibali na baadhi ya wanafunzi kudaiwa kusoma kozi kadhaa bila kuwa na sifa stahiki.
Makalla ameitaka menejimenti kuwarudishia wanafunzi fedha walizolipa kama ada. Hata hivyo, mmoja wa viongozi wa chuo hicho aliwekwa chini ya ulinzi na hatimaye kuchukuliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi.
Wanafunzi walipatwa taharuki huku baadhi yao wakizimia baada ya agizo la Makallla la kukifunga chuo hicho ambacho awali kilikuwa kikijulikana kama Ihemi Polytechnic College.
Pamoja na gharama walizoingia, wanafunzi wanalalamikia muda waliopoteza kusoma masomo ambayo hayatambuliki na kuitaka Serikali walau kukubali vyeti ambavyo wamevitapa chuoni hapo"