Rc Mbeya avunja uongozi wa soko la sido, na mfanya biashara atakaye goma kusaini mkataba atapitisha greda kuvunja vibanda walivyojijengea

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Sido

Kwa ufupi
Leo Jumatano, Oktoba 24, 2018, Mkuu Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameuvunja uongozi wa wafanyabiashara Soko la Sido kwa kile alichodai, viongozi hao walikuwa wanawadanganya wafanyabiashara na kuwashawishi kutolipa kodi kwa masilahi yao binafsi.

By Godfrey Kahango, Mwanachi gkahango@mwananchi.co.tz
Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameuvunja uongozi wa Wafanyabiashara wa Soko la Sido jijini humo kwa kile alichodai, viongozi hao walikuwa wanawadanganya wafanyabiashara na kuwashawishi kutolipa kodi kwa masilahi yao binafsi.

Chalamila ametoa uamuzi huo leo Oktoba 24, 2018 alipofanya mkutano wa hadhara na wafanyabiashara hao ndani ya soko hilo kwa lengo la kutoa msimamo wa Serikali juu ya mgogoro uliopo baina ya wafanyabiashara na uongozi wa Jiji la Mbeya kuhusu kodi ya vibanda vya maduka.

Pamoja na kuvunja uongozi huo, Chalamila pia ameruhusu kufunguliwa kwa maduka yote yaliyokuwa yamefungwa kwa amri yake kwa lengo la kushinikiza wafanyabiashara hao kulipa kodi ya Sh50,000 ya vibanda pia kila mfanyabiashara awe na leseni ya biashara na Tin Namba.

“Kwa muda mrefu viongozi hawa wamefanya kazi ya kutapeli watu (wafanyabiashara) lakini ndio walikuwa wakishinikiza wafanyabiashara kutolipa kodi huku wakiwachangisha fedha.”

“Nimewaita waje ofisini kwangu tuzungumze kuhusu utaratibu mpya wa kuanza kulipa kodi tukazungumza nao na walipoondoka wakaniandikia barua ya kunishtaki kwa Waziri Mkuu kwamba mimi (Chalamila) ninawanyanyasa na sasa wametupeleka mahakamani,” amesema Chalamila.

Alisema baada ya kufunga maduka yote na kutamka kwamba kila mfanyabiashara anayetaka kufanya biashara aende Jiji kwa ajili ya kusaini mikataba upya, tayari wafanyabiashara zaidi ya 500 wamefanya hivyo na bado wachache ambao aliwapa muda hadi kesho Ijumaa wawe wamekwenda kusaini mikataba na kama hawatafanya hivyo basi atapeleka greda na kubomoa vibanda hivyo.
 
Sugu kaa pembeni watu wafanye kazi .

Inasikitisha mno majiji yanayoongozwa na Chadema ndiyo yanayoongoza kwa kukwepa kodi ,ulaji rushwa na utapeli.

Kwa kasi hii mkuu wa mkoa nakutabiria makubwa.
 
Hongera RC ,ni lazima na wajibu watu walipe kodi stahiki. Ili jiji na Serikali kuu ipate mapato sitahiki kwa maendeleo.
 
chalamila anachowafanyia sido sio kizuri....nimegundua huyu sio kiongozi ila ni mbabaishaji
 
Back
Top Bottom