RC Manyara atoa maelekezo kwa Ma-DED na DMO

RC Manyara atoa maelekezo kwa Ma-DED na DMO

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti ametoa maagizo kwa wakurugenzi watendaji wa Halmashauri.

Kuhakikisha wanatoa kipaumbele kwa wanachama wa mfuko wa BIMA ya afya iliyoboreshwa iCHF ili iwe chachu kwa wananchi kuhamasika wananchi kujiunga na mfuko huo.

Viongozi hao wameelekezwa kuhakikisha Kuwa wanachi wanahamasishwa kupitia Mikutano rasmi ya vijiji na ya hadhara kujiunga na iCHF ili kutikia asilimia 50 ifikapo Desemba 2019.

"Nawaagiza Wakurugenzi wote mukawashirikishe wakuu wenu wa Wilaya katika mikakati ya kuongeza usajili wa kaya kwenye mfuko huu ili kila wilaya ifikie angalau asilimia 25 ifikapoJuni 2019 na asilimia 50 mwezi Desemba 2019"Alisema mkuu Mkoa

Aliyasema hayo leo tarehe 29.11.2018 kwenye ukumbi wa white Rose ulioko mjini Babati wakati akifungua kikao cha kujadili mwongozo mpya Wa iCHF Wa Kitaifa ambao umeboreshwa kutoka kwenye mfumo uliokuwa ukitumiwa na mikoa ya kaskazini ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Wajumbe Wa kikao hicho walikuwa wenyeviti Wa Halmashauri, Wakurugenzi watendaji Wa Halmashauri Zote za Mkoa Wa Manyara na waganga Wakuu Wa Wilaya pamoja na waratibu Wa iCHF Wa Wilaya
 
Back
Top Bottom