RC Makonda, kabla ya kuingilia ndoa za watu muulize kwanza Augustino Lyatonga Mrema alipoishia

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Hawa ni akina mama na watoto wao wamefika leo kwenye ofisi za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakidai kutelekezwa na wazazi wenzao.




Wakati Lyatonga Mrema akiwa waziri wa Mambo ya ndani alianzisha deski la akina mama kueleza matatizo waliyonayo kwenye ndoa zao.

Nakumbuka Mrema alikuwa akiwapa siku 7 wanaume waliotelekeza familia zao kuripoti ofisini kwake.

Walipofika ofisini kwa Mrema wanaume wengi walikuwa wakiomba kesi zipelekwe mahakamani. Kesi nyingi ziliamuliwa zikasikilizwe nje ya mahakama kwa sababu pesa ya matunzo ambayo ingeamuliwa na mahakama isingekidhi mahitaji ya wakati huo.

Mahakama ilikuwa bado inaitambua sheria ya ndoa ya mwaka 71 kuhusu matunzo ya mtoto kuwa ni shilingi mia (100) kwa mwezi.

Hadi leo sheria hiyo haijabadilishwa.

Sina uhakika Makonda amejiandaa kiasi gani, lakini ningeshauri kama kweli ameamua kuwasaidia ajenge ushawishi kwa bunge kubadili sheria ya ndoa kuendana na mazingira ya sasa. Vinginevyo anaenda kuongeza matatizo juu ya matatizo.
 
Kwanza hii kazi ilipaswa kufanywa Na Wizara ya mambo ya Ustawi wa Jamii

Nashangaa Makonda mpaka kwenye page yake ya Instagram ana post akina Mama wa Mikoani waliokuja kwake wakati yeye anahusika Na wa Dat pekee!

Mie nasubiria Kwa hamu Sheria atakayotumia Makonda kushughulikia Wanaume wenzangu!

Pia ange deal Na Wanawake waliotegeshea Mimba
Mie nimemlipa anipe Mzigo nitambae yeye anategeshea Mimba
 
Kwanza hii kazi ilipaswa kufanywa Na Wizara ya mambo ya Ustawi wa Jamii

Nashangaa Makonda mpaka kwenye page yake ya Instagram ana post akina Mama wa Mikoani waliokuja kwake wakati yeye anahusika Na wa Dat pekee!

Mie nasubiria Kwa hamu Sheria atakayotumia Makonda kushughulikia Wanaume wenzangu!

Pia ange deal Na Wanawake waliotegeshea Mimba
Mie nimemlipa anipe Mzigo nitambae yeye anategeshea Mimba
Lengo kuu la Makonda ni kupewa wizara ndio maana yuko bize kupost wanawake wa mikoa mingine.
 
Poor Planning. siku zote vituo vya kusaidia wanawake wenye matatizo kama haya vipo wazi. Madawati ya jinsia yapo, ustawi wapo kila kona na hata taasisi za haki za binadamu zipo. Sasa hii kurupuka kurupuka maana yake nini? hilo rundo la kina mama watasaidiwa vipi zaidi ya kupewa maelezo na vipeperushi tu?

Zaidi ya kutumia vibaya raslimali za nchi, hii ni kuwapotezea mda watanzania kwa kuwarubuni kuwapa msaada. Siku zote Bashite simkubali. Kila afanyacho ni kukurupuka tu.
 
Sina uhakika Makonda amejiandaa kiasi gani, lkn ningeshauri kama kweli ameamua kuwasaidia ajenge ushawishi kwa bunge kubadili sheria ya ndoa kuendana na mazingira ya sasa. Vinginevyo anaenda kuongeza matatizo juu ya matatizo.


Huko hawezi kwakuwa alishawanyea mikono sidhani kama watamwona analo la maana
 
Huyu mtoto anaonekana wa jamii ya kichina itabidi Makonda ampe mama yake nauli akamtafute mzazi mwenzie China kazi kweli kweli.
FB_IMG_1523276142068.jpg
 
Wanakuwa wajuvi wa kupanua mapaja, ikiingia mimba wanalia lia wametelekezwa. hapo naona mnafanya mtu flani awe maarufu tu lakini hakuna jambo la maana, zaidi kuna wanaume watakabidhiwa watoto walee wakati sio wao maana DNA itakuwa imedukuliwa kuleta majibu ya Yes sir.
Pole wanaume maana hatunaga mtetezi kisiasa, wanasiasa wanaogopa kukosa Kura wakisema ukweli
 
Back
Top Bottom