RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

kama kuna video footage basi Bashite yupo in trouble!
Njaa zinakuvuruga, na mwisho wa Maisha ya mwajiri wako ni april pale mjengoni
=====
Msomaji, vema pia ukasoma hapa > Mwanamama kupitia Uhuru FM, adai kuzalishwa na Askofu Gwajima na kutelekezwa!
=====



Makonda hua anafika office za clouds mara kwa mara. Siku zingine anashinda hapo mpaka jioni. Siku ya Alhamis Makonda alifika office za Clouds Cha ajabu siku hiyo alikaa mpaka usiku akawa anamtafuta soudy Brown na Qwisser wa SHILAWADU muda huo walikuwa bado hawajafika kazini basi akawa anazungukazunguka tu ofisi hii anatokea ile kama mfanyakazi wa Clouds.

Kwenye Mida ya Saa kumi hivi akakutana na kina Soudy pamoja na prodyuza wa kipindi wakawa wanaongea kwa uficho hivi na usiri tukajua tu ni mambo ya kawaida ya kuhitaji uprivate lakini siku ile ulikuwa unatia mashaka sana.

Kumbe Makonda alikuja na Story ya mwanamke mmoja ambaye yeye Makonda alisema huyo mwanamke amezaa na mchungaji Gwajima na ametelekeza akawa anataka arekodiwe na ubuyu uruke kwenye kipindi cha SHILAWADU.

Basi wakakubalia kwa kuwa ni habari itabidi huyo mwanamke arekodiwe na kipindi kiruke siku ya jana lakini kawaida ya Kipindi cha SHILAWADU ubuyu ukipatikana lazima kila mtu apewe Natural Justice ya kusikilizwa pande zote mbili sababu huwa ndiyo kawaida ya kipindi.

Makonda siku hiyo hiyo ya Alhamisi akamwambia Soudy ajiandae then huyo mwanamke mnayemuona kwenye video na mtoto aliletwa na wasaidizi wa Makonda ahojiwe na Soudy Brown tayari kwa kurushwa kwa kipindi.

Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni jana SHILAWADU wakamtafuta Gwajima kwa upande wake kama anaifahamu hiyo ishu na je mwanamke huyo aliyetajwa ni kweli kwasababu tunaelewa ugomvi uliopo kati ya Makonda na Gwajima isijekuwa SHILAWADU wanatumika kuwafitinisha watu vibaya!

kwa bahati mbaya Gwajima hakupatikana jana ijumaa kwa ajili ya kurekodiwa na kufanyiwa mahojiano.

SHILAWADU wakatumia busara mpaka apatikane Gwajima scene ya Dada mwenye mtoto ziende kwa pamoja na ya mchungaji Gwajima kama kawaida ya POVU inavyokuwaga.

Jana usiku sasa kumbe Makonda alikuwa anafuatilia kipindi cha SHILAWADU aone kama kile kipande kitaruka hewani wapi ndiyo akaamua kuja Clouds na magari mawili yeye mwenyewe Makonda na Watu kama nane hivi wakiwa na Bunduki aina ya SMG geti la kawaida mlinzi alifungua geti kwasababu amezoeleka Mh anakujaga mjengoni wakafunguliwa kisha wakaingia ndani.

Walipofika reception wakazuiwa kuingia ndani sababu hatuna utaratibu wa kuruhusu wageni baada ya saa Nne usiku kuingia ndani ya Ofisi kama siyo mfanyakazi wa CLOUDS.

Alipoona wanazuiwa wakatoa bunduki zao mlinzi akashurutishwa afungue mlango kwa nguvu sababu walimtishia na Silaha mlimzi akafungua mlango wakaenda naye hadi studio kipindi kilikuwa kinaendelea hewani.

Makonda akawatoa nje Soudy na Mwenzake Qwisser akawauliza kwanini video aliyowaletea haijachezwa wakaelezea utaratibu jinsi utaratibu ulivyokuwa Qwisser wakati anajielezea akapigwa mtama akaanguka chini wakavamia mitambo ya transmission kwenye traycaster wakitaka kile kipande kirushwe hewani prodyuza wa kipindi akamuambia Makonda kwanini anavunja utaratibu na kutumia nguvu na ameshapewa utaratibu akapigwa na kitako cha Bunduki mgongoni akaanguka chini bahati mbaya kipindi kilikuwa kimefika mwisho.

Wakamshurutisha Prodyuza wa SHILAWADU anaitwa Chriss awape kile kipande wakaondoka naye wakati wanaondoka Ruge alikuja na Polisi akaingia lakini tayari walikuwa wameondoka ofisini wamechukua hicho kipande cha Video ya huyo mwanamke.

Hizo video zilichukuliwa kwa nguvu na Makonda na hao watu waliokuwa na Silaha inasemekana Makonda ana timu yake wanazisambaza kwa kasi na hatujui lengo lake ni nini.

Hata mkihitaji footage za Camera zipo jinsi tukio lilivyokuwa usiku wa jana.

====
Kutoka kwa wadau wa Clouds Media


Habari kama hizi za kichochezi na za uzushi ndizo zinazotuponza wanaJf mbona tuliokuepo mjengoni mda huo hatujasikia lolote na hakuna chochote kilichotokea.

Au umetumwa?
Clouds ni taasisi kubwa inayoongozwa kwa misingi na taratibu zake haiwezekani mtu from no where aje tu aingie mpaka peoduction bila kufata utaratibu!

Acha uzushi watanzania puuzeni hizi taarifa si za kweli!!.
 
sasa ni ukweli usio shaka kuwa kuna vita kubwa sana dhidi ya paol Makonda na imefikia hadi watu wanatangeneza kudai video eti kuuaminisha umma kuwa ni makonda kwenye iyo video. Jamani achani propaganda uchwara na kwa taarifa yenu hizo propaganda zenu uchwara ndo zinasababisha magufuli awaone hamna la maana zaidi ya vita binafsi dhidi ya makonda.
Mliotengeneza video hiyo mlichokosea ni kuwa Mkuu wa mkoa halindwi na askari wanaovaa mabaka mabaka(kwa tanzania ni JWTZ), pili ni kuwa Jeshi Polisi Tanzania halina nguo za mabaka mabaka kama kenya na tatu ni kuwa Jwtz hawajihusishi na shughuli za usalama zilizoko chini ya polisi. Alafu how comes JW waende clouds wameshika bunduki alafu polisi asishike bunduki????? kweli kitengo cha propaganda dhidi ya makonda na mange wenu. Period.
Sawa le mutuz
 
Ni kashfa kubwa kuwahi kutokea ktk historia ya nchi hii mkuu wa mkoa kuvamia chombo cha habari akiwa vikosi vya ulinzi na usalama na kufanya fujo studio, mamlka zinazousika tukianzia na chama cha mapinduzi, wizara uhusika na TCRA zitatoa tamko gani, lkn kote uku tusingefika kama hatua stahiki zingechukuliwa mapema.
 
Naona Mange kaposti extended version video. ikionyesha askari zaidi wakiingia

hii Vita imefika patamu sana.
 
Habari kama hizi za kichochezi na za uzushi ndizo zinazotuponza wanaJf mbona tuliokuepo mjengoni mda huo hatujasikia lolote na hakuna chochote kilichotokea.

Au umetumwa?
Clouds ni taasisi kubwa inayoongozwa kwa misingi na taratibu zake haiwezekani mtu from no where aje tu aingie mpaka peoduction bila kufata utaratibu!

Acha uzushi watanzania puuzeni hizi taarifa si za kweli!!.

baada ya ushahidi kuwekwa nadhani ni uungwana ukaomba samahani!
 
9c084a1a13feeb7f728b8af6459b29fd.jpg
Saa 4 usiku akiwa na majambazi wenzake.


Hapo kuna lipi la kushangaza? Ni kiongozi na analindwa.
 
kwa kweli nahitaji kujua LeMutuz ana akili timamu au vipi. maana naona amesimama kidete eti anapinga hii video anasema RC alikiwa na walinzi wake wa kawaida kabisa
 
Mch. Gwajima: Albert Daudi Bashite
alipata ZERO Kidato cha Nne na
kila somo alipata F! Wiki ijayo
nzima ntakuwa kazini dhidi yake
 
Habari kama hizi za kichochezi na za uzushi ndizo zinazotuponza wanaJf mbona tuliokuepo mjengoni mda huo hatujasikia lolote na hakuna chochote kilichotokea.

Au umetumwa?
Clouds ni taasisi kubwa inayoongozwa kwa misingi na taratibu zake haiwezekani mtu from no where aje tu aingie mpaka peoduction bila kufata utaratibu!

Acha uzushi watanzania puuzeni hizi taarifa si za kweli!!.
Kwa Mara ya Kwanza nimeanza kuamini kuwa JF ni Mtandao Makini Kabisa, Mimi ni Mfanyakazi wa Clouds Media Group, Nipo Marketing department. Mwanzo Tulikua tumezuiwa kueleza Ukweli wa Hili Jambo, lakini Kutoka na Maadili ya Uandishi imebidi wakuu wa Idara waruhusu lizungumzwe, Leo Asubuhi Karibu wafanyakazi wote wamezungumza kuhusu ukweli huu. Ninasikitika sana kuona watanzania wajinga kama wewe Kubisha kitu ambacho hukijui halafu unadanganya Umma kuwa Ulikuwepo Mjengoni, huu ni Unafiki wa Kijinga. Jamaa yako kafanya Tukio kweli, na Mbaya zaidi aliyekua anambeba na kuendekeza huu Ujinga wake ni boss Ruge, lakini kwa mara ya kwanza Baada ya Kikao cha Jana Kizito Kapigwa marufuku, wafanyakazi wote tumefurahi maana tulikua tumemchoka na Tabia zake hapa Ofisini utafikiri yeye ndo Boss wetu. Kiufupi aliyezuia ile Video ya Mama mwenye mtoto ni Sisi wote kama Idara, tulimuomba ufanyike Uchunguzi kwanza ili kubalance Stori kabla haijaruka. Sasa Kaka, hayo ni Machache tu, Makonda ajitokeze Akanushe halafu sisi tutaweka Ushahidi wote.
 
Habari wanabodi. Kwanza hongereni sana TLS kwa Uchaguzi sahihi na makini, bila shaka yeyote mmeweka historia.
Lengo la uzi huu ni kuweka wazi mienendo na dalili kwamba kelele zenu juu ya uwajibikaji,uwazi na utawala bora zinakwenda kupata majibu. Tuhuma juu ya Daudi Albert Bashite/Paul Makonda inakwenda kupata njia ya kuanza kumshitaki mahakamani kwa makosa mbalimbali likiwamo hili la jinai.
Nyakati kadhaa tumeona mahusiano kati ya Paul Makonda,Magufuli na Clouds Media. Na mara nyingi JPM amekuwa akitumia Clouds Media kuzungumza na Paul Makonda katika mikutano ya hadhara,na hakusita kuwapongeza wote. Juzi tu amepiga tena simu na kuongea na diamond, na kusema kwamba ni mpenzi wa kipindi cha umbeaumbea. Baada ya tukio la uvamizi wa clouds, na kutolewa kwa video footage ni wazi sasa Clouds na Makonda si marafiki tena na ukizingatia tabia ya kisasi aliyonayo. Hii unakuja baada ya ushahidi kuwekwa wazi juu ya kupora mali za watuhumiwa wa madawa ya kulevya. Nyakati zimefika.Walioonewa ni muda wao kuanza kuitafuta haki.
 
Back
Top Bottom