RC Makonda atangaza kiama kwa wanaume wanaowapa wanawake mimba kisha kuzikataa

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,456
17,219
Habari ya wakati huu wakuu.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mheshimiwa Makonda amewatangazia kiama wanaume wote wanaowamimba wanawake kisha kukataa mimba au kukimbia mimba.

Amedai atashughulika nao kadri awezavyo, atapambana nao hadi ahakikishe kua wawe wanatoa matumizi ya mimba na mtoto.
Screenshot_20171117-081841.png

Hili nyie mnalionaje?
 
Pale unapotaka kupambana na mwanaume mwenzako ni lazima ukwame.... Awe tayari kupima DNA za Mtoto aliyeko tumboni na mwanaume anayehisiwa kutoa mimba...hatuaminiani siku hizi...awe makini hapo...
Km ameishiwa idea aseme tumsaidie kumpa ili aendelee kuweka mambo mengine saw a aachane na upande huu wa mimba. Awe anashauri watu wake wa Dar wasizae ovyo hadi pale wanapoona wanauwezo wa kuhudumia familia zao. Maana wengi huzaa alafu wanashindwa kulea...(awe mshauri na sio kupambana nao)
 
Hivi anafikiri kuweka mimba ni sawa na kufoji vyeti? Au mama wa vito vya thamani kampelekea mashtaka.. Tamaduni zetu sisi wa pemba na wasukuma ni kuzaa na ni sifa mojawapo ya kiume.
 
Inabidi awaambie na wanawake waache kulengesha mimba kwa watu ambao hawana mpango wa kuwaoa, maana wengine hufanya hivyo ili kuwanasa waume za watu pasipokuwa na makubaliano maalum
 
Mweshimiwa una mashine ngapi za DNA?
Zitakazoyusaidia kubaini kuwa mwenye mimba ni yeye?

Una wataalam wangap wa DNA ? ni kila mkoa au DAR tu?

Mweshimiwa kwa kuwa nchi hii kwa sasa hakuna mhimili wa mahakama unaosimamia uthibitisho wa vipimo nakuhakikishia linawezekana,
Maana mwanamke akisema nmepewa mimba na fulan na hakuna uthibitisho wa kitalamu bali mabavu tu hilo litawezekana.

Mweshimiwa angalia usijechemka.
 
Tatizo hao anaosema omba omba wengi wanatoka mikoani pia sasa sijui ataenda na huko kuwakomesha maana vitu vingine hata hujui useme nini ukiwa unakurupuka kusema kitu upate airtime lakini utekelezaji sasa .....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom