VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kwa mujibu wa Ripoti ya Kamati Maalum ya Waziri Nape Nnauye juu ya 'ujambazi' uliofanyika Clouds Media, RC Makonda aliwatishia wanakamati kuwajumuisha kwenye skendo ya madawa ya kulevya. Wengine, wafanyakazi wa ofisi yake, akawatisha kuwa 'watamjua yeye ni nani'. Hapa kuna jambo kubwa.
RC Makonda, kulingana na kilichoelezwa na Kamati ya Nape, amejianika kama kiongozi anayeendesha mambo yake kwa hila, inda, visasi na chuki. Amejianika kuwa hata yale Majina ya watuhumiwa wa Madawa ya Kulevya yaliandikwa na kutajwa kimkakati na katika hali isiyo na ukweli wowote.
RC Makonda amejianika kama kiongozi anayetumia vitisho na kujiamini kwakuwa tu yuko top anayemlinda na kumpa kiburi. RC Makonda hapaswi kuaminiwa tena. Kamati ya Nape imemuanika na sasa watanzania wanamjua na watamfuatilia. Ina maana kuwa yeye, kwa ulevi wake wa madaraka, huingiza watu kwenye kashfa au kuwasweka rumande kwa hila.
RC Makonda amejianika katika rangi yake halisi. Haaminiki tena na sanaa yake ambayo bado hajaimudu vyema.
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam