RC Makonda ahamia kwenye kikapu

RC Makonda ahamia kwenye kikapu

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,286

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA leo ametoa msaada wa Generator ya kisasa, Mabati 150 na Mipira 110 kwa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es salaam ili kujengea uwezo timu ya Mpira wa Kikapu ya Mkoa.

Generator hiyo ya kisasa ina uwezo wa KV 35 na haitoi mngurumo wa sauti (silent) ambapo ikijazwa mafuta inaweza kutumika kwa muda wa masaa nane mfululizo.

RC MAKONDA amesema anataka kuona Timu ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam inakuwa timu kubwa itakayotoa Wachezaji wakubwa wanaocheza ligi za ndani na Nje ya Nchi.

Uamuzi wa RC MAKONDA kugawa vifaa hivyo ni baada ya kualikwa kwenye ligi ya mchezo wa Kikapu Uwanja wa Taifa na kujionea Uchakavu wa Bati unaosababisha Wachezaji kunyeshewa na Mvua, Ukosefu wa Generator umeme ukikatika na uhaba wa Mipira hali iliyokuwa ikiwapa wachezaji wakati mgumu.

Aidha RC MAKONDA aliahidi kujenga viwanja vitatu vya Mchezo wa Kikapu ambapo tayari ramani imetengenezwa na muda sio mrefu atasaini mkataba na mkandarasi wa ujenzi wa Viwanja hivyo.

Ili kuendelea kuimarisha Michezo Dar es salaam RC MAKONDA anaunda kamati maalumu ya kushughulikia michezo ya aina zote.

Tayari RC MAKONDA amepata mdau atakaejenga Swimming pool la kisasa Kinondoni kwaajili ya Mchezo wa Kuogelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa kikapu Dar es Salaam OKARE EMESU amemshukuru RC MAKONDA kwa msaada wa vifaa hivyo pamoja gharama za mafundi.


Muungwana
 
Wakati wengine wanataka maneno wenzio wanafanya action..hapo ndipo unaona umbali wa ardhi na mbingu
 
Kijana wewe unatembea kwenye footsteps za boss kubwa no stories, tangible tu
 
Sijui nani huyo kashawekewa zengwe na ili asalimike basi atoe jenereta na mwingine mabati!
 
Hongera Makonda. Ni aibu nchi kukosa modern indoor arena for basketball/volleyball/handball/netball. Ushauri wangu fanya hivyo viwanja vya kikapu viwe multi-games court.
 
afu atasema serikali haijatoa hata kumi , je fedha zimetoka wapi?somebody got bullied
 
Huyu choko kashindwa kumpa mwanamke mimba kwa Miaka 6 kazi kuuza sura sijui anashughulikiwa yeye?
 
Back
Top Bottom