RC Makonda aandaa Iftar kwaajili ya wakazi wa Dar es salaam

Serikali haina pesa kwa sasa huyo makonda anapata wapi PESA ya kufutulisha umati mkubwa kiasi hicho na huku mtaani wauza mboga mboga wanakabwa kulipia vitambulisho
 
Batili tupu haya mambo ni kinyume na dini ya uislamu kabisa.Tangu lini mkristo akamfuturisha muislam ni aya gani katika Quran au hadithi sahihi iliyoelekeza hivyo?
Masheikh wanauelewa uislam kamwe hawawezi hudhuria tamasha hilo
Kuna watu wanatumia nguvu kubwa sana kuonekena ni wasafi mbele ya jamii na kutumia shida za watu kama ngazi ya kisiasa
Hakuna shida mkristo kumfuturisha muislam mkuu, wala hakuna tatizo wala kukatazwa katika dini ya usilam kusaidiana na wasiokuwa waislam. Kwa mfano kutoa sadaka unatakiwa umpe alie muhitaji tu, haikutajwa lazima awe na dini gani.
Tatizo hapa ni huyo mfuturishaji mwenyewe, ana lengo gani la kutoa futari hii? Kwa ninavyomuelewa mhusika hakika nisingependelea kushiriki katika futari hii!
 
Na ibada kabla ya kufutari ilipatikana kweli,ama walifutali na ibada ikafuata baadae
 
Batili tupu haya mambo ni kinyume na dini ya uislamu kabisa.Tangu lini mkristo akamfuturisha muislam ni aya gani katika Quran au hadithi sahihi iliyoelekeza hivyo?
Masheikh wanauelewa uislam kamwe hawawezi hudhuria tamasha hilo
Kuna watu wanatumia nguvu kubwa sana kuonekena ni wasafi mbele ya jamii na kutumia shida za watu kama ngazi ya kisiasa
Umenena kweli tupu.
Jambo la pili ni kuwa unawafuturishaje watu wenye futari (wenye uwezo) badala yakuwachukua maskini.Haya yote ni kujionyesha na Waisamu wenzangu sijui kwa nini tunashindwa kukemea haya
 
Kwani ni aya ipi inayomkataza muislamu kufuturushwa na mkristo?
Ni jambo la busara kama tutakuwa tuna focus kwa suala la kufuturisha badala ya kukejeli dini,kwani dini zote zipo kwa maana na lengo kuu moja ni amani
 
Back
Top Bottom