RC Hapi akemea utendaji wa kimazoea Iringa

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
894
Reaction score
994
*RC HAPI AKEMEA UTENDAJI WA MAZOEA IRINGA*

*Aagiza watumishi wa serikali kupimwa kwa matokeo ya kazi wanazofanya kila wiki*

Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Wafanyakazi wa serikali Mkoani Iringa wametakiwa kutoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu yao kila wiki yakionesha jinsi walivyotatua kero za wananchi katika maeneo yao.

Agizo hilo lilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Ally Hapi alipokuwa akiongea na wafanyakazi wa Wilaya ya Mufindi katika ukumbi wa CCM mjini Mafinga leo.

Mhe Hapi amesema kuwa kila wiki mfanyakazi atoe taarifa fupi ya kazi alizofanya na kazi anazotarajia kufanya wiki inayofuata ili kufuta utendaji wa mazoea katika Mkoa wa Iringa.

*"Nataka tuwe na mfumo wa utoaji taarifa za utendaji kazi kwa wiki, kila mtumishi aeleze kafanya nini wiki iliyopita na atafanya nini wiki inayofuata.Ili tujue nani anafanya kazi na nani hafanyi tuchukue hatua, na wisho wa mwezi tupokee mishahara ya halali."*
alisisitiza mhe Hapi.

Katika utekelezaji wa agizo hilo, wakurugenzi wote ikiwemo wa halmashauri ya mji wa Mafinga na Wilaya ya Mufindi waliagizwa kusimamia utekelezaji huo kwa kuanzia na wakuu wa idara.

Aidha, aliwakumbusha wafanyakazi hao kuwa kipimo cha kazi wanazofanya ni utatuzi wa migogoro na kero za wananchi na sio kigezo cha mahudhurio kazini pekee.

Mkuu wa mkoa alisema kuwa anategemea kufanya ziara ya siku 18 ya kutembelea tarafa kwa tarafa itakayokwenda kwa jina la *IRINGA MPYA*
*“Nitatembelea miradi ya maendeleo na kufanya mikutano mitatu kwenye kila tarafa. Katika ziara hiyo nitasikiliza kero za wananchi na kila mtandaji atajibu kero za eneo lake. Tutajua nani mla rushwa, nani mzembe na nani mchapakazi.Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe... "*
alisisitiza mhe Hapi.

Aliongeza kuwa kutokana na wafanyakazi kutotimiza majukumu yao, wamekuwa wakizalisha chuki kwa serikali iliyo madarakani kutokana na kushindwa kutatua shida za wananchi. Alisisitiza kuwa hatakuwa tayari kuwavumilia wafanyakazi wanaozalisha chuki na kuifanya serikali ya awamu ya tano ichukiwe na wananchi. Hapi amewataka watendaji kuwaheshimu na kuwasikiliza wananchi wanaofika kwao.

*“Kumekuwa na tabia ya kuwadharau wananchi na kuwajibu hovyo wanapohitaji huduma katika ofisi zetu. Watendaji ngazi ya vijiji, kata na ngazi zote lazima watenge siku ya kusikiliza kero za wananchi”*
alisema.

Mkuu wa mkoa wa Iringa yupo katika siku ya pili ya ziara yake ya kutembelea wilaya za mkoa wa Iringa na kufanya vikao na wafanyakazi na wazee kuelezea dira ya uongozi wake katika falsafa yake ya ujenzi wa *Iringa mpya.*
Akiwa njiani kurejea Iringa mjini, RC HAPI alisimama kuwasalimia vijana wa stendi ya Mafinga.
 
ANAJISUMBUA, BADALA YA KULIPA WATU STAHIKI ZAO AREAZ, WALIIPANDISHWA VYEO NA STAHIKI ZINGINE PAMOJA NA KUPANDISHA MADARAJA ANALETA SIASA,
HAKUNA MWENYE MORARI WA KUFANYA HIVYO ANAJISUMBUA TU
 
Anakurupuka hajui vichwa vya wafanyakazi wa serikali, hakuna mwenye moyo wa kufanya hivyo ningemwona wa maana angemwambia bosi wake alipe wafanyakazi stahiki zao
 
Nguvu ya soda iliyo tikiswa

Mwisho wa siku mtukufu wetu ataangalia kama mapato ya mkoa
 
Si ana kadi tu ya CCM huyo? Do he have any managerial expertise to set and evaluate employees by KPI's??
 
Alisimama kuwasalimia watu stenidi.
Mbona umesahau kuandika breakast na lunch yake na dinner
 
Back
Top Bottom