Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 757
- 1,822
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameeleza kwamba Jiji la Arusha halina uwezo wa kifedha wa kutekeleza miradi yoyote ya maendeleo kwani miradi yote inayojengwa kwa sasa katika jiji la Arusha inatekelezwa na serikali kuu.
Gambo ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa wadau wa benki ya CRDB unaofanyika katika hotel ya Kitalii ya Mount Meru jijini hapa na kuwataka wananchi waachane na upotoshwaji unaoenezwa na baadhi ya viongozi kuwa miradi hiyo inajengwa na jiji la Arusha.
Amesema kuwa jiji la Arusha linakusanya mapato ya sh,Billion 20.6 lakini gharama za mishahara ya wafanyakazi wake ni sh, bilioni 37 sasa utaona jinsi gani ambavyo halmashauri hiyo haiwezi kuendesha mradi wowote.
Gambo amesema kuwa miradi mikubwa ya kimkakati katika jiji la Arusha ukiwemo mradi wa maji wa bilioni 524,na ujenzi wa vituo vya afya inatekelezwa na serikali ya Rais Magufuli huku akiwataka wananchi waache kudanganywa na kupotoshwa juu ya miradi hiyo.
"Kuna miradi ya barabara inayotekelezwa katika jiji la Arusha ambayo imesainiwa yenye thamani ya shilingi bilioni 26 kwa ajili ya kujenga barabara zote za jiji la Arusha fedha ambazo zimetolewa na serikali " amesema Gambo.
Amesema baadhi ya watu wanaendekeza unafiki ,porojo na uongo juu ya miradi hiyo ,kumbuka ukiwa mnafiki bado kijana ukifikia umri mkubwa utakuwa mchawi"
Gambo aliishukuru benki ya crdb kwa ushirikiano wake wa kifedha katika ujenzi wa miradi mbalimbali mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na serikali hapa nchini.
.......