tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Agosti 22, 2025 ametangaza motisha ya Shilingi milioni 20 kwa wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kuelekea mchezo wa robo fainali ya Michuano ya CHAN dhidi ya Morocco, unaotarajiwa kupigwa usiku huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Chalamila amesema fedha hizo zitakabidhiwa kwa wachezaji bila kujali matokeo ya mchezo huo. Aidha, ameeleza kuwa motisha hiyo imeambatana na viwanja viwili vilivyopo Kigamboni ambavyo pia vitatolewa kwa timu hiyo.
Amefafanua kuwa kwa kila goli litakalofungwa, kiasi cha Shilingi milioni 5 kitatolewa. Mfungaji wa bao atazawadiwa Shilingi milioni 1, huku mtoaji wa pasi ya bao akipata Shilingi laki tano.
Chalamila amesema hatua hiyo inalenga kuongeza morali kwa wachezaji wa Taifa Stars katika mchezo huo muhimu dhidi ya Morocco.