WAKATI nyota wa muziki wa Hip Hop ,
Rashid Makwiro Chid Benz akikamatwa
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere akiwa na madawa ya kulevya akiwa
njiani kuelekea Mbeya, Rehema Chalamila
Ray C aliyekuwa amemfungulia kesi ya
kumpiga katika kituo cha Polisi cha
Oysterbay, amefuta shauri hilo na
kumsamehe.
Akipiga stori na gazeti hili , Ray C alisema
ameamua kumsamehe kwa sababu yeye ni
mtu wa Mungu na anaamini yanayomtokea ni
ishara ya kumtambulisha kuwa matumizi ya
dawa za kulevya hayafai .
Mimi ni mtu wa Mungu , nimemsamehe na
wala sitaki kesi naye , lakini kumsamehe mimi
peke yangu hakusaidii , Watanzania wote kwa
pamoja tumuombee ili jambo hili limalizike na
likiisha, ninamuomba aje tushiriki pamoja
katika tiba ya Methadone, alisema .
Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa
kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika
waraka katika akaunti yake kwenye mtandao
wa Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana
na matumizi hayo ya madawa ya kulevya .
Nyota wa muziki wa Hip Hop , Rashid
Makwiro Chid Benz .
Pole kaka yangu Chid Benz, naumia kuona
tatizo ulilokuwa nalo bado haujalitafutia jibu,
mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi
pamoja . Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa
nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua
na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia
kukushauri badala yake ukaja na rungu la
kimasai na kunitandika nalo nyumbani
kwangu , yalisomeka baadhi ya maandishi
yake mtandaoni .
Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo cha
kukamatwa kwake na madawa hayo kitakuwa
ni jibu zuri kwake kuwa anakoenda si salama
na kumtaka abadili njia na kuungana naye
kwenye tiba ya Methadone kwani ndiyo
kiboko ya madawa ya kulevya.
Kamanda Nzowa .
Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za
madawa ya kulevya pamoja na misokoto
miwili ya bangi hadi gazeti hili linakwenda
mtamboni , alikuwa bado hajafikishwa
mahakamani kukabiliana na tuhuma hizi