Rav4 slow acceleration

Zvi

JF-Expert Member
Oct 1, 2012
624
382
Habari wakuu!
Gari Rav4 1996 engine model 3S-GE ina tatizo la kuongeza kasi (acceleration), inaanza vizuri kutoka 0-50, baada ya hapo inajivuta sana kwenda 60,70 na 80. kupata spidi 100 inakuwa ni shughuri hata ukikanyaga peda mpaka mwisho kunakuwa hakuna mwitikio, kwenye milima/miinuko inasinzia kama vile inataka kuzima haf baadaye ina pick up ila mzunguko wa engine unakuwa mkubwa sana na engine inakuwa inapiga kelele. Nafikiri tatizo ni kwenye kubadili gia (sina uhakika). Nimebadili spark plugs, transmission oil, fuel filter na hakuna badiliko lolote, sasa naona mafundi wanakisia tu tatizo hawana uhakika thus why nimeona nilete hapa maana naamini sitakosa wataalam wa kunishauri au watu waliowahi kukutana na tatizo hilo.
Natanguliza shukrani!
 
Usingeishia kufanya engine service ungefanya na gearbox service pia,
seems kuna gia zinasumbua kuingia
 
Upo mji gani kakaa?!
 
Hata Mimi Nina vits 2005 inatatizo Hilo niliileka kwenye computer wakasema nozel nimebadili bado tatizo liko wanasema pump,nimechoka Saiz ishakula hela mingi
 
Usingeishia kufanya engine service ungefanya na gearbox service pia,
seems kuna gia zinasumbua kuingia
Kivipi mkuu? fafanunua. Nahisi tatizo litakuwa kwenye gear box lakini mafundi wanashindwa kabisa kutambua hilo
 
Jaribu Air Cleaner Sensor. Huwa kuna kijisensor kidogo sana pale kwenye Aircleaner. Kijisensor hicho kinaweza kuisinzisha gari pia. Kinasafishwa kwa pamba stick za masikio. Otherwise Shusha Gear Box weka mpya. Laki 6 tu kama ni front wheel na 1m kama ni 4 wheel
 
Safi nitakutumia nmb ya bingwa wa toyota cars, Toyota Japan trained, atakusaidia sana, my Corona premio ilikuwa na tatizo kama hilo, I will be back
Nitashukuru sana mkuu
 
Jaribu Air Cleaner Sensor. Huwa kuna kijisensor kidogo sana pale kwenye Aircleaner. Kijisensor hicho kinaweza kuisinzisha gari pia. Kinasafishwa kwa pamba stick za masikio. Otherwise Shusha Gear Box weka mpya. Laki 6 tu kama ni front wheel na 1m kama ni 4 wheel
Nashukuru kwa ushauri
 
Pole sana kaka hilo tatizo nilikuwa nalo pia. Gari yangu Grande Mark II Gx 110. Mafundi wakawa wanajaribu jaribu lakin fund mmoja alifanikiwa tulibadili kitu kwenye engine, kinachozunguka shida ilikuwa ni kwamba meno yamepanuka kwa hiyo mzunguko wa engine uneenda tofauti. Ni pm nikupe namba ya mtalaam, akueleze vizuri
 
Kaka na ya kwangu ina shida kama hiyo
 
Pole sana kaka hilo tatizo nilikuwa nalo pia. Gari yangu Grande Mark II Gx 110. Mafundi wakawa wanajaribu jaribu lakin fund mmoja alifanikiwa tulibadili kitu kwenye engine, kinachozunguka shida ilikuwa ni kwamba meno yamepanuka kwa hiyo mzunguko wa engine uneenda tofauti. Ni pm nikupe namba ya mtalaam, akueleze vizuri
Nimeku pm
 
Jaribu pia kutumia petrol fuel treatment kwa ajili ya kuzibua fuel jets kwenye mfumo wa mafuta, inawekwa unapoweka mafuta siyo chini ya lita 30, Total wanayo nzuri bei ni 10,000 tu. Pia jaribu kubadirisha fuel filter ni ya chuma itakuwa inauchafu mwingi likishindikana hilo la kwanza.
 
Nashukuru kwa ushauri, nitajaribu hiyo hiyo fuel treatment, fuel filter nilibadilisha na nozzles walicheck zilikuwa zikitema mafuta vizuri
 
Back
Top Bottom