Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,513
- 8,276
Rais wa Cuba Raul Catro alifanya ziara fupi huko Vatikan Jumapili ili kumshukuru Papa Francis kwa juhudi zake za kumaliza miongo mitano ya mvutano kati ya Marekani na Cuba wakati nchi hizo mbili zikirudisha uhusiano wa kidiplomasia.
Kiongozi huyo wa Cuba alikutana na Papa mzaliwa wa Argentina kwa karibu saa nzima wakati watu hao wawili wakizungumza katika lugha yao ya asili ya Kihispania.
Papa Francis kiongozi wa kanisa Katoliki duniani alikuwa nguzo muhimu katika mazungumzo ya faragha kati ya Havana na Washington yaliopelekea tangazo la Desemba kwamba nchi hizo mbili zinachukua hatua ya kufungua tena ofisi zao za ubalozi katika miji yao mikuu na kupanua ushirikiano wao wa kiuchumi. Vatikan imesema Papa Francis ambaye ni wa kwanza kutoka Amerika Kusini , binafsi alikua mpatanishi kati ya pande mbili hizo na kuwa mwenyeji kwa wajumbe wa nchi hizo mbili.
Ya kwangu: ona ni furaha iliyoje nchi zinapata zikiwa na uhusiano na marekani kiasi cha kiongozi kufunga safari kwenda kumshukuru mpatanishi. Sasa ni muda wa papa kuelekeza nguvu zake kuzipatanisha na marekani zile nchi nyingine ili ziache kuishi kwa wasiwasi, make kwa wasiwasi walionao tunaona hizo nchi zinatumia muda mwingi, akili nyingi na nguvu nyingi kutengeneza siraha badala ya kutengeneza vitu ambavyo vingewapa faida kubwa, huyo ambae wana wasiwasi nae yuko busy anatengeneza magari, ndege, mziki mzuri, filamu nzuri, mitandao ya computer, wanamchezo, nk na kuuza worldwide then anapata pesa za kutengeneza uchumi na siraha. Papa shawishi iran, n.korea, russia, nk wapatane na marekani ili wafaidi utamu wanaoupata japan, s.korea, Qatar, china, nk
Ebu linganisha n.korea adui wa marekani na s.korea rafiki wa marekani, jibu unalo.