Ratiba ya wiki, jinsi ya kupost kwenye mitandao ya kijamii

Asiliatz

Member
Aug 16, 2018
97
131
Habari ndugu wananchi,.

Kitu kigumu uwa ni kupanga ratiba, kazi yakuitekeleza huwa sio ngumu sana kama ukipanga ratiba inayotekelezeka.

Hapa nimekusaidia kupanga ratiba ya wiki nzima nini unapaswa kupost kwa biashara yoyote ile.

Siku 2: jumatatu na jumanne ni kwaajili ya wateja, hapa fikiria zaidi maisha ya wateja wako, na upost kitu kinachogusa maisha yao.

Siku 2: Jumatano na Alhamisi ni kwaajili ya biashara yako, jielezee lengo la biashara yako kwa wateja na pia inadi biashara yako.

Siku 3: ijumaa, jumamosi na jumapili hizi ni siku za kuuza, jitahidi siku hizi kushawishi wateja wanunue unacho uza.

Hiyo ndio formula niliyoipa jina 2-2-3

Watu wengi siku zote saba wanatumia kuuza tu, kuonesha tu kile wanacho uza, tambua kwamba mitandao yakijamii sio kwaajili yakuuuza tu, inamalengo mengine mbali na biashara.

Husisahau pia sherehe za kitaifa na matukio yakitaifa ni vyema kuya post.

Kama umependa post hii ya mamilioni lakini unaisoma bure hapa

Like na share kusambaza upendo kwa wengine pia wafanikiwe katika biashara zao.
ratiba1.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom