Ratiba ya Utoaji heshima za Mwisho na kuaga mwili wa Alfonce Mawazo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,494
54,906
Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo Alphonce Mawazo

Kesho Siku ya Ijumaa Novemba 27 saa 2 asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo, eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA, wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo.

Baada ya Viwanja vya Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda.

Baada ya wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za mwisho.

Makene

============

Updates;

Pumzika kwa amani kamanda wetu Mawazo damu yako italeta ukombozi .
Poleni sana wafiwa wote
Hakuna giza linashinda nuru.
 
So sad! Pumzika kwa amani kamanda na rafiki yangu Mawazo
 
Ageni mwili wake kwa amani, hatutaki fujo hapa mjini. Na hao vingozi wenu muwaambie kuwa uchaguzi umeisha, lowassa peke yake aruhusiwe kuhutubia maana hawezi chukua zaidi ya dakika tano kuongea.
 
Ageni mwili wake kwa amani, hatutaki fujo hapa mjini. Na hao vingozi wenu muwaambie kuwa uchaguzi umeisha, lowassa peke yake aruhusiwe kuhutubia maana hawezi chukua zaidi ya dakika tano kuongea.

Uwezo wa kufikiri ndo umeishia hapo.
 
Ageni mwili wake kwa amani, hatutaki fujo hapa mjini. Na hao vingozi wenu muwaambie kuwa uchaguzi umeisha, lowassa peke yake aruhusiwe kuhutubia maana hawezi chukua zaidi ya dakika tano kuongea.

Wewe ndo ulihusika nini? Lazima albadri isomwe kuwalaani wauwaji, hakika hawataishi kwa amani hapa duniani, watakuwa wa kuweweseka, mizuka na majini yatawandama na ukoo wao. Allah sema na hawa wauwaji...
 
Ageni mwili wake kwa amani, hatutaki fujo hapa mjini. Na hao vingozi wenu muwaambie kuwa uchaguzi umeisha, lowassa peke yake aruhusiwe kuhutubia maana hawezi chukua zaidi ya dakika tano kuongea.

majebere;
Naamini weye umeshajilaani mwenyewe hivyo hata tukikulaani tunapoteza nguvu bure. Pamoja na hayo unayodhani unayafaidi kwa maneno yako hayo, lakini naamini wewe utakufa vibaya kuliko huyo Mawazo uliye muua. Hata maiti yako haitaonekana iagwe. Pole sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…