Quinine Mwitu
JF-Expert Member
- Oct 19, 2014
- 5,528
- 6,085
Wasalam,
Nimeona leo niwasifie hawa watu jamii ya rastafarian. Ni watu amabao walio wengi wana uzalendo wa kweli wa kulipenda Bara la Afrika na watu wao kwa mapenzi makubwa kabisa.
Ukitaja jamii ambayo huwa wanaichukia biashara ya utumwa mpaka leo, biashara iliyosababidha maumivu makubwa kwa watu wa bara la Afrika, basi huwezi kuacha kuwataja watu jamii ya rastafarian na mtu yoyote aliyeutukuza na kuwatukuza waafrika huwa wanampa kipaumbele kikubwa sana.
Mfano mpaka leo wanamchukulia Marcus Gavey kama Mtume wao kwa kuwa tu alifanya juhudi kubwa za kuwarudisha waamerika weusi kwenye bara lao, Afrika.
Na wanamchukia sana Mwafrika aliyeko ugenini ambaye hataki kutambua Afrika kama chimbuko lake. Wana msemo wao kuwa if you are a black man, wherever you are Africa is home.
Wameingia kwenye Mgogoro wa kudumu na Mapapa wote, point yao wanadai kama papa alikuwa muadilifu na muungwana asingeamuru jeshi la Italy kwenda kuivamia nchi ya Ethiopia. Walio wengi wanaamini kizazi cha Haile Selasie ndio kizazi cha mitume wote kwa kuwa Haille Selasie alikuwa mjukuu wa Mfalme Daudi, kwahiyo wao wanaamini hata Yesu Kristo alikuwa Mweusi ni watu weupe tu wameipotosha Historia na kumfanya yesu kama mzungu lakini si kweli.
Watu kama Akina Suni Ali, Walter Rodney, Martin Luther na waafrika waliofanya vyema miaka hiyo hadi sasa katika kutetea utu wa mtu mweusi bila kujali rangi zao nk, maana huwa wanamsemo wao mmoja wanasema you can have a white face with a black heart and viceversa. Mpaka leo, kwao bado unabaki shujaa wa mtu mweusi haijalishi rangi yako.
Yawezekana wakawa na Mapungufu, ila hili la uzalendo na mapenzi kwa Afrika huwa linanifanya niwakubali sana hawa watu na mtu yoyote atakayehujumu maisha ya mtu mweusi kwao ni msaliti mkubwa ''Babylon''.