MWANAHARAKATI MWEMA
JF-Expert Member
- Dec 16, 2022
- 235
- 335
Habari wana jamvi mimi namshukuru muumba wa mbingu na ardhi, mimi ni mfanyakazi wa idara fulani nina miaka zaidi ya kumi kazini, kuna ndugu yangu mmoja mzanzibar alinifundisha kamari [betting] mwaka 2015.
Tokea nimeanza kubeti kuna mambo mengi nimejifunza kutokana na michezo hii, mimi nakadilia kwamba nimeshapoteza pesa kiasi cha kati ya tsh 5,000,000/= hadi tsh 10,000,000/= kwa kipindi cha miaka kumi niliyoingia kwenye urahibu huu.
Katika kipindi chote hiki cha kucheza mchezo huu nimekula kiasi kisichozidi tsh 2,000,000/= na kutokana na nature ya kazi hii kuna mambo mengi nimehisi yanahusika na yanasababu.
[1]upangaji matokeo
Kwenye hili mutakubaliana nami kwamba kuna uhuni mwingi kuanzia wamiliki wa timu,wachezaji,marefa,makocha hawa wote wanashiriki kupanga matokeo kutokana na ofa za mabosi wa kampuni za kamari.
[2]UCHAWI
Najua wengi hamtaamini hili lakini ukweli ni kwamba ukibeti mkeka kuna mambo mawili yatakutokea usingizi wa ghafla mkeka unapoenda kuchanika ili husicash out, kucashout kwa hofu mkeka unawini hapa jini linakuamsha ata kama ulilala fofofo na mara zote dakika zikiwa za jioni. Hapa pana mambo mengi lakini ngoja niishie hapa.
[3]mizozo ya kifamilia
mara nyingi sana wacheza kamali wanakuwa wanazozana sana na familia zao hasa mke kwa sababu nyingi ikiwemo kutumia muda mwingi kufuatilia mkeka kuliko kushiriki tendo, matumizi mabovu ya pesa hapa unakuta mtu kapata pesa ya mshahara anawaza kwamba abetie mshahara ili apate mara mbili yake alafu amalize shida kinachokuja kutokea ni tofauti kabisa anakutana na uchawi wa muhindi analiwa pesa na nyumbani hakuna maitaji anaingia kwenye madeni.
Na uzoefu wangu kwa kwenye pesa ya mshahara ukibetia ni ngumu kula imeshanitokea mara nyingi sana ndio maana natoa ushuhuda ata kama ni timu moja tu.
[4]msongo wa mawazo
Mara nyingi watu wanaobeti wanapitia msongo wa mawazo sana kwa kuwa kula ni malachache kuliko kuliwa yaani unaweza kula laki mbili leo kesho unaliwa laki tano. hivyo wakamalia ujikuta mudabwote wanatukana kimoyomoyo na hasira za hapa na pale na wakati mwingine kuongea pekee yako pale inapotokea timu moja ndio imechana mkeka au timu kubwa inaharibu sherehe.
[5]madeni
mara nyingi wanaobeti wamekubwa na madeni katika maisha yao kwa sababu pesa zao hazidumu anakula leo kesho analiwa hivyo ujikuta awezi kuwa na akiba ya kudumu na anafujasana pesa, akiliwa anatamani kuweka mkeka mwingine hivyo ujikuta kila leo ni kuamisha pesa kutoka bank kuja kwenye simu mpaka zinaisha .
[6] ni wachache sana waliofanikiwa kwa kubeti 5% ya 100%
Ili si la kubisha ni ukweli mtupu huu ni ulevi mbaya na hauna faida yoyote kwa mtu anayejipenda na anajali afya yake aache mara moja kwa kuwa inadumaza akili za watanzania huwezi kupata watu wenye mfano wa mafanikio ya betting zaidi ya wale waliwekwa kwa kurubuni wenzao kwa matangazo ya kushawishi.
Mwisho sio kwa umuhimu kamai ni dhambi na inamadhara kiafya kuanzia leo nimefuta kila kitu kinachousiana na kamali kwenye simu yangu nikipata elfu kumi natumia buku 9 naweka nitakuwa na nifhamu na pesa yangu aliyeanzisha betting sio mjinga alishaona wapi na wapi pa kufanya upate pesa hasa wamewekeza kwa wachezaji, marefa na makocha.
Kwaherini wakamaria wenzangu mimi yamenishinda wewe je?