Rasimu ya katiba yashindwa kupunguza madaraka ya raisi

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Watanzania tumelalamika sana kuhusu madaraka makubwa ya raisi, tukaingia katika mchakato wa katiba mpya ambao tulitegemea madaraka ya raisi yatapunguzwa kwa kiasi kikubwa ili kuleta ustawi wa jamii. Ni masikitiko makubwa kuona madaraka ya raisi karibu yamebaki vilevile. mfano tunasema uongozi wa nchi una mihimili mitatu lakini kwa mujibu wa rasimu ya katiba mpya tuna mihimili miwili tu, yaani serikali na bunge. huwezi kuita mhimili wa mahakama ambao wakuu wake wote wanateuliwa na raisi kuwa mhimili wa uongozi wa nchi sambamba na serikali yenyewe. tumeunda katiba mpya tunahitaji mhimili muhimili wa mahakama kuwa chombo huru kinachojitegemea kutoa utatuzi wa migogoro ya kiutawala wa nchi lakini kwa mapendekezo yaliyotolewa mahakama inakuwa taasisi ya serikali hivyo hatuwezi kutegemea haki pale serikali itakapokiuka misingi ya katiba yetu na raia au taasisi zikakimbilia mahakamani kutafuta haki. hivyo ni bora tume ikaliona hili kuwa madaraka ya raisi ni makubwa kiasi cha kumeza mhimili mmoja wa uongozi. faida za kuweka mihimili mitatu ya uongozi kila mmoja ukijitegemea na nguvu zake ni kupunguza kiburi cha mhimili mmoja wapo, mfano bunge likitoa maadhimio yao na serikali ikayapuuuzia nini kinanyika, au mahakama ikitoa maamuzi na serikali ikayapuuzia nini kinafuata? lakini tukiwa na mihimili mitatu iliyohuru huu ukipuuzwa unakimbilia kwa mwingine na sauti zikizidi na bila woga serikali inaweza kufuata. Cha kusikitisha zaidi ni kuwa raisi anateua kila kitu. hili limekuwa tatizo kubwa watu wanaunda mitando kumbeba mtu aingie ikulu akiishaingia anawateua waliombeba kushika nyadhifa za uteuzi hata kama ni wahuni. tatizo hili ndilo linaloleta vita sehemu nyingi maana mgombea mwenyewe hawezi kuanzisha vita anaposhindwa ila wapambe wanaokuwa wanamsapoti ili kuteuliwa mara nyingi ndio hawakubali kushindwa kambi yao. lakini pia ili kuleta ufanisi ufanisi katika utendaji wa serikali maana tumeona raisi anamteua mkurugenzi wa shirika ambaye yuko chini ya waziri, waziri anashindwa kumuwajibisha mteule wa raisi au mkurugenzi anakwenda kumshitaki waziri wake kwa raisi badala ya kuripoti kwa waziri. tupunguze haya madara ya raisi kuteua kila kitu iwe ni raisi anateua waziri katika wizara na waziri anateua bodi kwa kulingana na sifa za kitaaluma na bodi inamuajiri mkurugenzi kwa kutumia maombi ya kazi. tuondoe utaratibu wa raisi kuteua kila kitu tulinde amani ya nchi yetu, tuondoe tabia inayojengeka ya watu kuatafuta kujuana badala ya kutafuta ujuzi, tuongeze ufanisi katika utendaji wa mashirika ya umma
 
eti raisi asishitakiwe! kama amefanya makosa ya wazi je suluhisho ni nini? au iwe kujichukulia sharia mikononi? huu ulikuwa utaratibu wa zamani Enzi za sasa viongozi wanashitakiwa mahakamani.
 
Back
Top Bottom