RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

where is the full document? hayo maeneo yote uliyoyagusia ni vague, the team did not do their work properly.

Pamoja na kwamba mimi binafsi sijaiona hiyo rasimu a Katiba mpya, kama alivyowasilisha mleta mada, nimevutiwa na mapendekezo ya kuwa na:

1. Baraza dogo la mawaziri wasiozidi 15 na wasitokane na Wabunge, sawa kabisa!

2. Spika na Naibu Spika wasitokane na Wabunge na wasitokane na vyama vya siasa, sawa kabisa!

3. Mawaziri, makatibu wakuu, Jaji Mkuu etc wathibitishwe na Bunge, sawa kabisa!

4. Jimbo likibaki wazi kusiwe na uchaguzi mdogo badala yake chama kilichopoteza kijaze nafasi hiyo, sawa kabisa!

Isipokuwa nakubaliana na mleta mada hii kuwa:

1. si sahihi Rais kuwa juu ya sheria, ashitakiwe kwa makosa ya uvunjaji sheria

2. si sahihi Mbunge akifukuzwa kwenye chama chake abaki na ubunge wake, akifukuzwa apoteze ubunge

Hayo ni maoni yangu pia.
 
Mwali ehh chondechonde punde unavyoipata,kwa niaba ya wadau wengi wenye uhitaji wa rasimu hiyo kama mim naomba utubandikie hapa pale utakapo ipata mkonon mwako hyo softy copy
 
This can't be fixed maana kila serikali ina prioritiews zake, wengine wanapenda kuweka mining na energy pamoja, next inaweza kuamua kuziachanisha etc. Sijui kama kuna nchi imeweka a fixed number.

Itakuwa vizuri na kama itaonekana haja ya mabadiliko waongeze kurugenzi kwenye wizara mama. Hii itasaidia kuwa na continuity na hivyo kuweza kuji-evaluate.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Leo wametaka serikari tatu kesho watazitaka serikari Nne yaani ya pemba,unguja,Tanganyika na ya muungano cha msingi Muungano ulipaswa uboreshwa kisasa zaidi
Uendane na wakati yaani serikari iwe moja tu hakuna lisilowezekana hapo maana ya kuboresha itaeleweka lakini kuleta serikari tatu ni kuludisha nyuma maendeleo tunaonba katiba mpya ije na serikari moja au majimbo
 
Rasimu hii bado mambo mengine yanahitajiufafanuzi, pamoja na viti maalumu kuondolewa lakini inapendekezwa kila jimbo litakuwa na wabunge wawili wa kike na kiume, sasa wanapatikanaje? au kila mgombea atakuwa na mgombea mwenza? wenye rasimu watfafanulie.
 
Kulifanya jeshi la polisi liwe huru tofauti na sasa ambapo polisi wanafanya kazi kwa hofu ya kutokiudhi chama kilichopo madarakani, hii ni lazima isisitizwe ili vyama viwe huru kufanya siasa pasipo vikwazo kutoka kwa jeshi hilo kama ilivyo sasa.
 
Nakuunga mkono rais asihusike kuteua majaji, tume ya utumishi ya mahakama ichague majina mawili ama matatu na yaingizwe bungeni kisha yapigiwe kura! Biashara ya rais kuteua wakuu wa mihimili mingine ya dola ni hatari kwa taifa letu!

Endapo chama chake kitakuwa na wabunge wengi itakuwa ni disaster. Tutarudi kulekule tunakokataa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mbwembwe tu, kutokana na hotuba ya Waryoba sijaona mambo ambayo yanawezakututia matumaini Watanzania.
Bila utekelezaji wa yaliyomo ndani ya katiba hata kama tukiipamba namna gani bado itabaki kuwa uchafu tu!
Msingi mzuri wa katiba nzuri ni kuwa na viongozi waadilifu na wenye uchungu na nchi, na wenye hisia za dhati kabisa ya kuleta maendeleo ya kiuchumi,kijamii, na kisiasa! Kuna matokeo mengi tu ya Tume nyingi tu na yaliyobeba ushauri mwingi na bora kwa serikali, lakini vinaozea maktaba za serikali!
:shock:It is just the beginning of wonders...!:shock:
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone

Wewe umeshaisoma hiyo rasimu na kukuta hayo mambo hayapo?

Hata kama hayapo kweli unaona kuna umuhimu wa kuweka kwenye katiba kutambuliwa Kiswahili kama lugha ya taifa?

Kama unataka Kiswahili iwe lugha ya taifa, hiyo mikataba itaandikwa pia kwa Kiswahili?

Halafu watu kama akina Prof Maji Marefu na Lusinde wanaweza kweli kujadili hiyo mikataba bungeni?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom