Bado nadhani wachangiaji wengi ama kwa kutokuelewa ama kwa makusudi tunadhani mzigo umepungua. Mwl.Nyerere aliona hili ndiyo maana aka sacrifice Utanganyika ili kuipunguzia mzigo serikali.
Tunapojadili hii rasimu, tukumbuke hii ni kwa masuala ya muungano peke yake, lakini pia tukumbuke kwamba Tanganyika itakuwa na bunge lake kama ilivyo kwa zanzibar, na mawaziri wake, n rais wake na utitiri wote tunaouona leo kwenye muungano.
Wengi tunadhani hii katiba itatusaidia, lakini ukiangalia kwa kutulia,hili laserikali tatu likipitishwa, tujiandae na maumivu mengine huko mbeleni.
Tuisomeni kwa makini lakini pia tusisahau kwamba tunachokijadili ni katiba ya muungano na siyo ya Tanganyika au ya Zanzibar. tunapojadili ukubwa wa bunge au udogo, tujue hilo ni la Muungano na siyo la Tanganyika au la Zanzibar.
Warioba katutega, nasi tumetegeka kisawasawa.