VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Chama chetu cha Mapinduzi kimejipanga,tangu mwanzo wa mchakato,kudhibiti mchakato na kulinda maslahi ya kichama. Kinaelekea kuweza. Kuyalinda maslahi ya kichama ni kulinda sehemu kubwa ya Katiba ya sasa ambayo 'inabeba' chama chetu. Pamoja na sauti zinazopazwa kila uchao na wapinzani na wanaharakati,Rasimu inakaribia kupitishwa. Chama kimejiandaa na kujipanga kufanikisha hilo.
Mambo yote yameshawekwa tayari.Ndiyo maana sasa Katibu Mkuu Kinana na ujumbe wake wanatembea pande za Tanzania kwa raha zao kujiandaa na uchaguzi ujao. Hawana hofu juu ya kupita kwa Rasimu. Itapita tu. Katiba 'mpya' itapatikana.
Amini nawaambia, CCM itayumba na kusawajika ikipitaRasimu hii. CCM itajuta bila mafanikio kudhibiti mchakato na kupitisha Rasimu. Itakuwa too late! Kila mwananchi amejiandaa kivyake. Kwasasa Polisi wanaogopwa. Ukifika muda, wananchi watatamba kwa kura zao. Itakuwa heri ungekuwepo kuona ninachokisema hapa.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam