William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,466
Sidhani kama Rashid Othman ana maagizo ya ku kuchunguza wizi wa hela. TUKUKURU na Tume Ya Maadili ndio kazi zao. Nadhani Rashid Othman hata majambazi wanaotishia maisha ya watu hawamhusu. Sio maagizo ya kazi yake.
Kwa wale wote mnaojaribu kumtetea Mkurugenzi wa Usalama, kutokana na shinikioz la baadhi yetu hapa JF kwamba ajiuzulu wakati muafaka ni sasa, kuhusiana na mapesa ya Chenge nje ya nchi yetu,
Ninaomba mjaribu kutafuta strong arguments za kumtetea, sio hizi mnazoleta so far,
1. Rais anapotaka kumchagua kiongozi, hapewi faili la yule kiongozi na Tukukuru, au maadili ya uongozi, anapewa na usalama wa taifa.
2. Takukuru na maadili, hawana maofisa hata mmoja nje ya nchi, yaani kwenye balozi zetu huko nje, walioko huko ni usalama wa taifa ambao walipaswa kujua kuwa Chenge anazo hizo hela huko nje, waliko tena wengi sana.
3. Mfano mdogo, kiongozi wa kwanza kuulizwa kuhusu hii ishu ya Chenge, alikuwa ni waziri wa usalama, Sophia Simba, sio mkuu wa Takukuru wala maadili, unafikiri ni kwa nini? Si huyu waziri Simba angesema sio kazi yao usalama, lakini umeona majibu yote aliyoyatoa kwamba yes ni yeye anyehusika, na kwamba alikuwa hajui kuwa Chenge ana hizo hela, lakini wameanza kumfuatilia na pia kushirikiana na wazungu wanaochunguza ishu,
Tatizo hapa ninalifahamu sana, wengi wa watetezi wake mnalalia udini, ingawa hamsemi tu lakini we know that tayari, ninawaomba kuwa mtafute strong argument za kumtetea Mkurugenzi, so far mnaleta vioja tu!
Ninarudia tena kuwa sasa ni wakati muafaka kwake mkurugenzi wa usalama kujiuzulu, ili kulinusuru taifa na hii ordeal ya ku-focus na mafisadi tu, tunataka kurudi kwenye ishus muhimu kwa taifa, sasa hatuwezi kwa sababu usalama wa sasa hauna uwezo wa kikazi ku-deal na viongozi mafisadi.
Ahsante!
Kwanza, Mama Simba sio Waziri wa Usalama. Na hiyo wizara haipo tena, imemezwa na Mambo ya Ndani chini ya Lawrence Masha. Hapo kwanza ushaanza kupoteza uaminifu; tunaanza kujiuliza kama unajua unachokielezea kwa sababu umejenga hoja kubwa kutegemea huu upotofu. Lakini wote tunakosea, hebu tuendelee.
Mabalozi wa nje hawana nguvu za kuingia kwenye akaunti inayo endeshwa kwa sheria za nchi ya kigeni. Ukiamini hivyo basi utaamini ki hekaya kilicho sambazwa humu FJ leo kwamba makachero wa Kitanzania wamemkamata mwana JF japo hawana jurisdiction, hawana sheria, ya kukamata mtu -hata Mtanzania - ndani ya Uingereza.
TUKUKURU na Tume ya Maadili ndio wamelala, sio Rashid Othman. Endelea kuongoza majeshi dhidi ya Ufisadi, Field Marshall ES. Tuko nyuma yako, lakini ukirusha mikuki kwenye wrong target tutashtuana!
Kwanza, Mama Simba sio Waziri wa Usalama. Na hiyo wizara haipo tena, imemezwa na Mambo ya Ndani chini ya Lawrence Masha. Hapo kwanza ushaanza kupoteza uaminifu; tunaanza kujiuliza kama unajua unachokielezea kwa sababu umejenga hoja kubwa kutegemea huu upotofu. Lakini wote tunakosea, hebu tuendelee.
Mabalozi wa nje hawana nguvu za kuingia kwenye akaunti inayo endeshwa kwa sheria za nchi ya kigeni. Ukiamini hivyo basi utaamini ki hekaya kilicho sambazwa humu FJ leo kwamba makachero wa Kitanzania wamemkamata mwana JF japo hawana jurisdiction, hawana sheria, ya kukamata mtu -hata Mtanzania - ndani ya Uingereza.
Tatu, unapoanza kuongelea dini kwenye usalama na rushwa unazika uaminifu ambao nadhani umeshakufa mpaka hivi sasa! Kitu ambacho kinanipa kichefu chefu hapa JF ni utitiri wa mi-thread ya kidini ambayo sijawahi kuifungua achilia mbali kuchangia- hata siku moja. Isitoshe nina dhambi nyingi kiasi kwamba nikianza kumtetea Mungu wa dini yeyote ile, yani atajisogeza mbali na mimi kuliko McCain alivyoikimbia endorsement ya Bush!
TUKUKURU na Tume ya Maadili ndio wamelala, sio Rashid Othman. Endelea kuongoza majeshi dhidi ya Ufisadi, Field Marshall ES. Tuko nyuma yako, lakini ukirusha mikuki kwenye wrong target tutashtuana!
Nani kasema kuwa Rashid hakumpatia JK habari za Chenge?? Tunaelekeza frustrations zetu pasipofaa. Wa kujiuzuzulu ni Kikwete, that is where the bucks should stop.
Sidhani kama ni tatizo kujua nani anyeeelekeza frustrations zake mahali pasipofaaa, waziri wa usalama amesema yeye alikuwa hajui habari za Chenge, meaning kwamba hata rais alikuwa hajui, halafu huna haja ya kuingia na majina mengi kueleweka hapa bro, tatizo lako la personal toka day one ni rais, hapana mkuu hiii topic inamhusu mkurugenzi wa usalama wa taifa,ambaye ameshindwa kufanya kazi yake inavyotakiwa, na ni vyema ajiuzulu now!
Hatutakubali kuwa distracted na maneno mengi empty!
MARK MWANDOSYA ameapa kutosubiri 2015...amedhamiria kuondoa utamaduni wa "kumwachia mwenyekiti"..kwa kuwa tayari ndani ya ccm kuna watu wa ndani wanaamini kuwa kuna kila dalili miaka kumi itakuwa mingi mno kikwete kuweza kuhimili..dhahiri kuna kila dalili kuwa anahitaji msaada...ameelemewa kabisa.......hata miaka 2.5 bado!!!!
Nafikiri unawatambua vizuri hawa wa usalama wa taifa, hata siku moja hawaripoti kwa mawaziri. Wao huripoti kwa mkurugenzi wao na yeye moja kwa moja kwa Raisi tu. Rashid hawezi kumshitaki Chenge kwa Simba, ili iweje? Nafikiri umefika wakati wa kutomuonea aibu Kikwete, ametuangusha na bila ya yeye kuondoka, uvundo utaendelea. The bucks have to stop at Kikwete's desk. Kwangu haileti maana yeyote kufukuza kila mtu ili tu JK abakie madarakani. WHY NOT LET JK GO????
with me problem haiko kwa RO, kwani nayeye anahitaji kutunza family yake, mambo yake ya kujirusha na totoz well that is too personal, as long as hafanyi kama mh.wetu wa bunge kutumia mali na pesa za idara kuhudumi hizo totoz, Akijiuzulu leo kwa kuwa hakusikilizwa (ukweli ni kuwa alifahamu na kutoa taarifa) halafu akawekwa mwingine na mchezo ni ule ule what is the point ya kujiuzulu? ili yasimkute yaliyomkuta kombe RIP)itabidi akae kimya na hivyo watanzania hawatajua kwa nini amejiuzulu and that will remove the whole meaning ya ku-resign.
what we need is the system change, question we need to ask ourselves and actions we need to take are, what part of the system is needed to be changed? why are we changing it? and how do we like it to be after the change? then we make noise to change that.
Rashid Othman si alikuwa field officer pale London kwa muda mrefu kabla ya kurudi nyumbani kupewa ukurugenzi?
Sasa kama field officer, alifanya nini kuhakikisha kuwa;
He RO is indirectly or directly responsible on this period. I do not understand the mumbo jumbo about it is not him or TISS responsibility to make sure that everything is done correctly and for interest of Taifa.
- Wakati wa kesi ya IPTL kwenye abirtration court, palipotakiwa ule ushahidi kuwa kuna rushwa ili mkatabe uvunjwe, kwa nini hakufuatilia kwa haraka na kuwapa wawakilishi wa Tanesco na Serikali ushahidi ambao ulipelekwa kwa Hosea ili Serikali ishinde kesi na hivyo kuachana na IPTL?
- Wakati Ndege Koko na Radar zinanunuliwa, agent na middleman alikuwa London. Je yeye RO kama field officer alifanya juhudi gani kuunganisha nukta na kutoa maoni yake kuhusiana na suala zima la Radar, mkataba wake, bei yake na alternative equipment?
- Kama field officer, alishindwa vipi kugundua safari za kila siku na dakika za mawaziri au watendaji kama Mramba, Chenge na Yona ambao wanatuhumiwa kwa Uhujumu na ufisadi?
- Akiwa field officer, alihusika vipi kuipa serikali intelligence report kuhusu Meremeta na Tangold ambazo ziliundwa kinyemela Uingereza na maafisa wa Serikali ya Tanzania na JWTZ?
It is not about corruption that he is responsible for, it is our National Security.
If our Attorney General was compromised to enter a dubious deal that not only did cost our nation billions of shillings but also the item purchased was not sufficient enough to provide adequate security coverage to protect our country, the he RO as to his previous position as Chief Field Officer and his current position as Director General of TISS he has failed our Nation!
His inaction or appearance of being unwilling to address the situation at hand with firmness has jeopardize security of our nation!
We are beating too much on this poor guy, Rashid,
1. Mkuu usalama wa taifa zamani ulikuwa chini ya wizara isiyokuwa maalum, kipindi cha mkapa ikahamishiwa wizara ya utawala bora, mpaka leo, kitine alishawahi kuwa waziri wake na bado mpaka leo ni ofisi ya rais.
2. Maofisa wa usalama wanaripoti kwa mkurugenzi wa usalama, depending on ths ishu, ikiwa too political ni lazima waziri wahusishwe, lakini kama haina politics kabisaa ni mkuurgenzi binafsi as mkurugenzi ndiye mwenye mamlaka ya kuamua what to do, anayo power ya ku-act na kumuarifu rais baadye.
3. Mafaili ya viongozi wote wa juu wa taifa yapo Ikulu, ambako katibu wa ofisi ya rais ndiye incharge wake, rais anapotaka kum-promote kiongozi ni lazima apewe brief na usalama wa taifa na pia kupewa faili lake ambalo hawa usalama wa taifa ndio wanahusika nalo as far as information zake is concerned.
4. Usalama wa taifa wana a strong hand kwenye ku-object kupewa madaraka kwa kiongozi yoyote yule nchini, kwa sababu walizozifanyia uchunguzi, Mwalimu wakati anamkataa Lowassa kugombea urais, alikuwa na information nzito za kifisadi against him ambazo alikuwa amepewa na usalama wa taifa,
kwa hiyo ni wajibu wa usalama wa taifa kuwa habari za Chenge, kuwa na mapesa yote hayo nje na jinsi alivyoyapata, kwa sababu nilitegemea kuwa utakuwa ni wajibu wa usalama wa taifa kujua kiongozi wetu wa juu huko nje ameenda wapi na kufanya nini,
Takukuru na maadili, wanaweza ku-cordinate info, na huwa wanafanya hayo kwa sababu ninakumbuka wakati wa uchaguzi wa rais 2005, maadili walikuwa na info nyingi za muungwana, akiwa nje ingawa 90% zilikuwa ni uongo wa kubuni, sasa maadili walizipata wapi hizo info? Zilitolewa na maofisa wetu wa usalama walioko nje,
Mimi nikiwa US huko nyuma, kulikuwa na ofisa mmoja wa usalama, aliyekuwa akinifuata fuata sana na kutuma ripoti nyingi za uongo bongo zinazonihusu, akifikiri kuwa ana akili sana kumbe mimi nilikuwa ninamchora tu, na kumuona mjinga kwa sababu wakati anahangaika na mimi, kulikuwa na viongozi kama hawa Chenge wakifanya mambo yao ya ufisadi sasa unaona kwamba hii ishu inaangukia wapi usalama wa taifa. Huyu mkulu alinisingizia kuwa nilimmualika mgombea mmoja wa urais na wazungu walihudhuria na kuchanga dola karibu millions ili kumsaidia yule mgombea, kitu ambacho ni uongo wa mchana na a pure nonesense, tena ninaweza hata kulitaja jina hapa na ujinga wote lilikuwa likiufanya na wake za watu, badala ya kuwafuatilia kina Chenge, sasa haya ndio matokeo yake tunakuja kuumbuliwa na wazungu, na hili li-ofisa nalo lifukuzwe kazi pia, tena najua liko wapi sasa, maana haya ya Chenge yamefanyika likiwa kule US.
Mkuu angalau kidogo una some sense, some of your points zinahitaji considerations.
Whaaat? Hivi unajua aliyemuachia ana mali kiasi gani bro? Eti mkulu ni poor guy? Kwani Chenge, hakuwa poor guy mpaka majuzi tu zilipotoka hizi info?
KJ, kama wote wanaomshauri Rais na hawasikilizi wakianza kujiuzulu mmoja mmoja labda ataanza kuwasikiliza wale wengine. Kama husikilizwi kwanini kuendelea na nafasi yako? Aidha ni waoga kuwajibika, wanapenda kuimba sifa za JK au ni wazembe kiutendaji. Huwezi kumshauri Rais kuhusu mambo muhimu akakupuuza na wewe ukaendelea kumshauri jambo jingine!
It is not for Rashid to take the ultimate fall, it is for Mr. President Jakaya Mrisho Kikwete.