RAS ni nani?

Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa ni sehemy ya Utawala na Rasilimali Watu ina jukumu la kuhakikisha kwamba huduma za kiutumishi na utawala katika mkoa husika zinatolewa kwa mujibu wa kanuni, sheria, taratibu na miongozo ya serikali. Miongoni mwa majukumu ya msingi ya sehemu hii ya utawala na rasilimali watu katika mkoa ni kama ifuatavyo;

Kuratibu masuala ya Mahusiano na Ustawi wa Wafanyakazi ikiwa na pamoja na masuala ya Afya, Usalama, Michezo na Utamaduni

Kuratibu maandalizi, utekelezaji, usimamizi na tathimini ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja kwenye Sekretarieti ya Mkoa

Kutoa huduma za Masijala, Ofisi na utunzaji na usimamizi wa kumbukumbu

Kutoa huduma za Kihitifaki/Itifaki katika Mkoa

Kuratibu huduma za Ulinzi, Usafi na utunzaji Ofisi, majengo na maeneo/viwanja vya ofisi na huduma za Usafiri

Kutoa huduma za ujumla za uangalizi wa vifaa vya ofisi na majengo

Kusimamia na kuimarisha masuala ya Nidhamu kwa watumishi ikijumuisha utoaji wa elimu ya kuzuia Rushwa.

Kuratibu utekelezaji wa masuala mtambuka kama Jinsia, Ulemavu, HIV/AIDS kwenye Sekretarieti ya Mkoa

Kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma – Tume/Sekretarieti ya Ajira juu ya masuala yote yanayohusiana na Ajira na Uteuzi wa watumishi.

Kuwezesha programu za mafunzo elekezi kwa waajiriwa/watumishi wapya.

Kushauri juu ya ufanisi wa kitaasisi wa Sekretarieti ya Mkoa

Kusimamia hatua/Mchakato wa kuwathibitisha na kuwapandisha vyeo/madaraja watumishi wa Mkoa

Kuwezesha mafunzo ya rasilimaliwatu na maendeleo (taaluma, weledi, kuboresha ujuzi) kwa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa.

Kusimamia Mpango wa Rasilimaliwatu kwa ajili ya kujua upatikanaji na mahitaji ya wataalamu kwenye Sekretarieti ya Mkoa.

Kusimamia mishahara na kushauri juu ya kusimamia mfumo/orodha ya malipo ya mshahara

Kusimamia utekelezaji wa mfumo wa wazi wa mapitio na upimaji wa utendaji wa kazi (OPRAS)

Kushughulikia na kuhuisha taarifa za watumishi kama Likizo za mwaka, likizo za uzazi na matibabu, ruhusa za mafunzo/masomo na watumishi kuondoka kazini.

Kuratibu upatikanaji wa mafao ya watumishi (malipo ya pensheni n.k) na madai mengineyo

Kushughulikia upatikanaji wa huduma zinazohusiana na watumishi kuondoka kwenye utumishi (kustaafu, kujiuzulu, kufariki n.k.)

Kuratibu kamati ndogo ya Ajira na Uteuzi ya Mkoa.

Kuratibu dawati la msaada na malalamiko

Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa juu ya masuala yanayohusu rasilimaliwatu

Kusimamia upatikanaji wa huduma za Habari, Elimu na Mawasiliano kwa ajili ya Sekretarieti ya Mkoa.

Kusimamia na kuratibu ziara zote za Viongozi wa Kitaifa na Mkoa zinazofanyika katika Mkoa wa Lindi.

Kuratibu utekelezaji wa sera ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na sheria nyingine zinazohusiana na Utawala na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika uimarishaji wa Muundo wa utekelezaji majukumu ya Sekretarieti ya Mkoa.

Kutekeleza majukumu mengine yatakayotolewa na Katibu Tawala Mkoa.
 
Back
Top Bottom