Rap Zenye Ujumbe

Rap Zenye Ujumbe

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
17,572
Reaction score
27,344
Wengi wanahusisha Rap kwamba ni miziki ya Kihuni inayo-glorify violence na uhuni.., lakini ni ukweli usiopingika kwamba Raps ukisikiliza zina ujumbe pia na nyingine zinatoa nasaha safi kabisa kwa jamii...

Mfano:- kwenye Nuthing but a G Thang.., Snoop anawahasa vijana kutumia contraceptives/condoms kuepuka magonjwa

From a young G's perspective and before me dig out
A bitch I have to find a contraceptive

You never know she could be earnin' her man
And learnin' her man and at the same time burnin' her man
Now, you know I ain't with that shit, Lieutenant
Ain't no pussy good enough to get burnt while I'm up in it


Tukija kwenye kuwaasa vijana / ma-blacks wanavyolalamika kuhusu watu weupe wanawakandamiza lakini pia inakumbuka kujiangalia wenyewe kuna hizi beti mbili moja kutoka kwa 2 Pac- Only God Can Judge Me na NonChalant Five O Clock in the Morning
I've been Trapped since birth, cautious, cause I'm cursed
And fantasies of my family, in a hearse
And they say it's the white man I should fear
But, it's my own kind doin all the killin here

I can't lie, ain't no love for the other side
Jealousy inside, make em wish I died
2Pac Only God Can Judge Me



NonChalant 5' O Clock in The Morning
Wella, Mr. Black Man tell me where you're heading
The last few years I watched while you were sheading
Pounds and pounds on growth for the population
Soon we won't be able to have a strong black nation
A shooting here, a stabbing there nowhere to stop
Cause now you're dying from the dose of the crack rock

I'm just a Nubian Queen that needs a king to stand strong
And try to press on
It's not a white man's finger on the trigger
Car-jacks, drive-by's, callin' each other "nigga"

I'm not here to scold but rather shape n' mold
That young black mind that won't live to grow old
Cause you're fronting smoking on the blunt and
Down with your friends cause you think you're making ends,
But you're not - and that's the truth of the matter
Your brother gettin' skinny, cause you want your pockets fatter


Camarades, tukumbushane Raps / verses zenye ujumbe - Nina uhakika kwenye pande hizi Verses za kina Fid Q pia hazitakosa (ingawa wavumao kina 2 Pac lakini kina Fid Q wapo
 
By Fid Q. nahisi anawaimbia wazee wa s2:-
Changanya akili ya kuelezwa na kile unachokifaham wema,
ukweli uwe mchungu kumeza na uwe mtamu kutema,
wengi mmebebwa mgongoni hamjui uchungu wa safari...
 
Artist kama JMO,FID Q ni darasa tupu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Artist kama JMO,FID Q ni darasa tupu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums



wengi leo wapo chali na walivuma ile kinoma jirushe kiakili kabla line light yako haijazima...Mo
 
GWM ft 2 Proud AKA Sugu "Yamenikuta"


Verse ya Sugu

Ukiishi kwa upanga na utakufa kwa upanga
Mungu ndio anapanga kila kitu kwa kila mtu
Yamenikuta mpaka najuta kuzaliwa
Heri ni nife
Kwanini nisife maisha haya
Dunia sio mbaya walimwengu ndio wabaya
Kujulikana kuna mambo, watakusema sema kila jambo
Hawakawii fulani H.I.V.
Wanapakaza hivi hivi​
Tukirudi kwenye mitaa ndio balaa hakuna raha
Polisi wanatughasi, utasema wanakisasi na sisi
Wanatamani watumalize kwa risasi
Kucheka nataka kulia nataka
Nabaki mdomo wazi
wasomi wamejazana hakuna kazi
Kilichobaki tukazane tu mabibi na mabwana
Kwani hatuna namna tena
Yamenikuta, yamenikuta yamenikuta
Na wengi yanawakuta yaliyonikuta
 
GWM ft 2 Proud AKA Sugu "Yamenikuta"


Verse ya Sugu

Ukiishi kwa upanga na utakufa kwa upanga
Mungu ndio anapanga kila kitu kwa kila mtu
Yamenikuta mpaka najuta kuzaliwa
Heri ni nife
Kwanini nisife maisha haya
Dunia sio mbaya walimwengu ndio wabaya
Kujulikana kuna mambo, watakusema sema kila jambo
Hawakawii fulani H.I.V.
Wanapakaza hivi hivi​
Tukirudi kwenye mitaa ndio balaa hakuna raha
Polisi wanatughasi, utasema wanakisasi na sisi
Wanatamani watumalize kwa risasi
Kucheka nataka kulia nataka
Nabaki mdomo wazi
wasomi wamejazana hakuna kazi
Kilichobaki tukazane tu mabibi na mabwana
Kwani hatuna namna tena
Yamenikuta, yamenikuta yamenikuta
Na wengi yanawakuta yaliyonikuta

HATAREEEE!!!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
By langa
Natumia akili, ustaarabu na subira
Situmii mwili, jazba na hasira
 
Nowadays maisha mafupi/kama urefu wa kibwengo
ukiendekeza kushusha chupi/hautatimiza malengo
Ukubwa sio kutoka jando/au kujua kutongoza
Ubishoo uweke kando/ukizubaa utakuponza
Tambua,ufanis wa kazi/hauj bila kujituma
Toa fikra za ubazazi/utozi na unyangema
Sawa ujana maji ya moto/basi yapoze kwa ibada
Na fataki usimkuze mtoto/kwa kumfanya kimada
Elimu chanjo ya ujinga/soma sana ukipata mwanya
Utadumu zaidi ya mninga/ usipopita njia za panya................YOUTH REMINDER BY ME,MYSELF AND I...Idriss Baraghash
 
Ingekuwa Vipi Mwana FA ft Jay Mo (kuanzia Beti za Mwisho Mwisho)
Mwanafalsafa
Ingekuwa vipi Bongo mitumba isingehalalishwa?
Masista Du pedal-pusher vipi wangeshonesha?
Jay Moe
Vitovu wangetuonyesha?
Je mapozi yangekwisha?
Au pigo gani brother-man leo zingemdatisha?


Mwanafalsafa
Ingekuwa vipi bongo wasingekuwepo changudoa?
Wateja wao, je wangewaopoa makaka poa?
Jay Moe
Au pengine matendo ya ubakaji yangewaingia?
Au labda ni masterbeshen ndizo zingewaokoa?

Mwanafalsafa
Ingekuwa vipi kasi ya Ukimwi kusingekuwa Condoms?
Yani ingekuwaje bila Ukimwi tungetinga Condoms?
Au Ukimwi ungekuwepo halafu hakuna Condoms
Unadhani mi ningesema mimi na mabinti ni dam-dam?

Jay Moe
Ingekuwa vipi ulipe buku tu kwa kila pumzi?
Kiumbe gani angediriki leo kupiga mluzi?
Unadhani ni watu wangapi wangekuwa wazima?
Labda tajiri, mafukara si tusingepona!

Mwanafalsafa
Ingekuwa vipi kama Bongo ingekuwa kama New York?
Washikaji wangejazana ubalozini kuomba viza?
Au viza tungezipata bila ya kuongea Kiingereza?
Kama sio chizi utawaza, maswali mi najiuliza.
Ingekuwa vipi?

KIITIKIO

Mwanafalsafa
Ingekuwa vipi Yesu angerudi?
Angemaliza vita ya Wapalestina na Wayahudi?
Fikiri ungeisha vipi mgogoro wa nchi ya ahadi?
Na fikiri uwepo wake ungeokoa maisha ya wangapi?

Jay Moe
Ingekuwa vipi kama Osama angeutawala Ulimwengu?
Wamarekani Uarabuni wangekuwa Sungusungu?
Je magaidi wangekuwa nani, ma-black au Wazungu?
Waarabu wangeelimika, wangetoka kwenye ukungu?

Mwanafalsafa
Ungekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini?
Dunia bila dhambi,Kipimo cha uovu nini?
Polisi, mahakama na gerezani angeenda nani?
Huitaji dini tathmini ingekuwa vipi hali ya amani?

Jay Moe
Vipi kama duniani wangekuwa ni mabinti peke yao?
Je wangetembea uchi kwa sababu hakuna wenzao?
Au wangejisitiri! Mitindo ingekuwa ya nini?
Ya kazi gani kama hakuna wanaume duniani?

Mwanafalsafa
Vipi kama Wazungu wasingeingia Afrika?
Nadhani maendeleo kwetu yangechelewa kufika.
Magari, ndege, Reli na nguo, nani angeleta?
Na bila biashara ya utumwa wangekuwepo black Amerika?
ah ha?​
 
Sihitaji Marafiki Fid Q

CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

VERSE :1
haijalishi ulikua na wangapi bali wangapi uko nao
..washkaji ambao... kosa lako lao wakati hauna mafao
wanaokufikiria wewe muda ambao
wenzao walionao wanafikiria wengine ndo wanao
now
kupata washkaji ukiwa na pesa... ni rahisi

kuwapata na hauna kitu ujue umefanikiwa kichizi mie sikufichi sihitaji urafiki na usupastaa
ukihit ndo unang'aa.. upishwe useat kwenye bar,upewe beat na Jr..
kitu ambacho haikuwa rahisi kipindi fid ni underground
sikuhizi mabinti wanaomiss ni walionidiss mie sio mdau

wanakubali mie ni mkali wanataka kuijua Mmwanza
ninayoitangaza nikiwa safari kama habari za kwanza

U-N-I-T na prof Ludi walionifunza kukaza...
kwetu mbali.. sijui lini nitarudi? (C) Lokua kanza

sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea
aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

VERSE 2;
na usupastaa huwa ni feki.. utakung'arisha ukiwa na Market

utakupatia senti,utapita juu ya red carpet

utageuka young & restless, utakupa wanawake
utakupa mafake brethrenz.. kisha utaenda zake
kwahiyo power its not permanent.. huwa ipo kwa muda tu
respect ur own conglomorete... fikiri kikubwa tu
masaa hayarudi nyuma kama muda wa kufuturu walioukataa utumwa wanastuka hawana uhuru

wanazusha najiskia.. so im my own best friend

sikia fidq anamsifia fareed ni bandidu sio Yes man

naweza nikakata ringi kiasi cha kutopay attention, lakini sio tajiri wakuafford kuua true friendship

tuweke siasa kando sababu kichwa kinanigonga
na hizi falsafa double double ajabu sio kinywa cha mjomba

sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea
aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

CHORUS
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani
Machizi sikusoma nao, tulikutana tu mtaani
udogoni sikucheza nao lakini ndo machizi wa ukubwani

VERSE 3
rafiki wa kweli yukoje.. ni mkimya au anayechonga
yule aliyekupa jina?au pengine anayekuponda? anayezuia usidondoke au anayesubiria kukuokota?
au ni yule ambaye ukimuudhi anakutusi kabla hajaondoka?
hakuna adui mbaya ka rafiki yako mwenyewe ambaye hajui.. ka yupo nawe.. au yupo kinyume na wewe
bora adui.. kama hachachawi utaenda muomba akuelewe

ka buibui.. naweka tandu mtaenda kando mzingue?

kwani machizi wenyewe wako wapi ambao wanastahiki niwape vyeo
inabidi tu uwaache wakuwatch kwenye kideo
unakula nao happy leo.. kesho wanamtaka mkeo
urafiki sitaki.. hauletagi maendeleo..

nilitamani kuwa mjamaa niwe genge kama nature

wachache niliowafanya wakang'aa wanayaweka maisha yangu in danger

sihitaji marafiki, labda baadaye wakitokea
aje mmoja wa kuongea nae, na mwingine wa kumuongelea

 
Sikilia Chunga Sana ya Salu T utaelewa kwa nini wanasema Hip Hop ya kweli haichezwi kwenye Radio
 
I am A Professional Fid Q

verse 3
Samaa X huniita Fid Q the future
machache niliyoyapitia kuna mengi nimejifunza, I am a professional
ruksa kunitoa ushamba kwa kile nisicho kijua
ntakuwa mjinga kwa sekunde kisha, I am a professional
nguvu ya elimu ina umuhimu pale elimu ikitumika
nalipwa kwa vyote ambavyo huvijui, I am a professional
muda mwingi niko sober kazi na sala kama mkoba
naamini Mungu ni mmoja ndo maana, I am a professional
tena im so grateful thankful, ili nipate mema natumia ufahamu, I am a professional
wanaongea walichosikia mi nasema nnachojua na sio ugly flow iko handsome, I am a professional
so usinitreat kama second class person utakuwa umefanya first class mistake hey, I am a professional
and im the best looking kama linen nikiwa mwendo kama Duke ukiwa kwenye mashine ah, I am a professional
HipHop ni vile unavyoishi rap ni kile unachofanya sikio la kufa zibuka usikie hizi dawa, I am a professional
katikati ya jana na kesho hapo ndipo kuna muda
kazi madeni kuzidi malipo mwiko mimi ni professional!
 
mistari ya wimbo wa jay moe STORI 3, au Langa anapoghani"kisichoniua kitanikomaza kiaskari, ukinichukia uathibitisha me ni mkali"
 
wimbo wote wa Afande sele uitwao HESHIMA akimshirikisha Chelea man ni darasa tosha. au wimbo wa Fid Q uitwao MWANANGU ambao amemshirikisha Banana zoro kwenye album ya VINA MWANZO, KATI NA MWISHO ni balaa
 
kufungua mawazo. funguo ngapi unazo?-afro reign saa za kazi kabla hujaharibu jaribu kinachokuhusu.......Mungu nipe Mungu nipe vitu vyote vya thamani. lakini ebwana eh kumbe Mungu sio athuman- hashim dogo- saa za kazi
 
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom