Rangi za msingi (primary colours) zenye hadhi, kueleweka na kuaminika duniani ni Nyekundu, Blue, Nyeusi, Kijani, Nyeupe na njano. Rangi hizi popote utakapozikuta duniani huwa zinatoa ujumbe unaoeleweka na kuaminika.
Nimeshangaa sana kuona chama kina bendera yenye rangi ya zambarau rangi ambayo ni ya kupumba kwa kuchanganya marangi mbalimbali na wala haielezi inawakilisha kitu gani hapa Tanzania, Afrika wala duniani. Nimetembea nchi 56 duniani sijawahi kuona bendera ya chama au taifa yenye rangi ya zambarau, labda bendera ya timu ya mpira ya Mbeya city na sare za sherehe za kitchen parties. Huu ni utani wa hali ya juu kwa watanzia waliosongwa na kero za maisha, maana rangi ya bendera inasaidia kutoa matumaini kwa watu waliokata tamaa. Rangi za bendera lazima zitoe ujumbe kwa wafuasi na kwawanaoitazama.
Nadhani hiki ni chama ambacho hakiaminiki sawa na rangi ya bendera yake. NI chama ambacho malengo yake hayaeleweki sawa na rangi ya bendera yake, hakina dira wala mwelekeo, kinatupumbaza wananchi ili tusahau tulikotoka, tulipo na tunakokwenda.