Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 20,541
- 41,293
Range ni muhindi piwaAnayesema range rover ni nzito kumbia anakaribia kuchanganyikiwa 😂😂😂
Weka land cruiser latest haifukuzi, weka Toyota fortuner latest ndo kabisaa, weka Nissan terra latest ndo itawaka moto 😄😄😄
Mpeni maua yake muingereza
Nadhani kukosekana kwa Highway Dar kumemfanya jamaa asijue speed ya Range.Anayesema range rover ni nzito kumbia anakaribia kuchanganyikiwa 😂😂😂
Weka land cruiser latest haifukuzi, weka Toyota fortuner latest ndo kabisaa, weka Nissan terra latest ndo itawaka moto 😄😄😄
Mpeni maua yake muingereza
Daaah pole mkuu ,chuma hatari sana Muingereza aliumiza kichwa hapo.Hii mashine ni balaa niliwahi kuwa na Ford Ranger ya 2023 mwaka jana maeneo ya Pahalapye,Botswana jamaa wawili walinipita na hizo chuma walikua nao wanaelekea daslm wale wale jamaa walinipita kama upepo na gari yangu dashboard inasoma speed 180km/h walinipita kama vile nimepaki gari wao walivuka mapema kazungula sijui hata kama walilala sehemu mpaka kufika Tunduma maana sikuwakuta nilisikia tu wamevuka..
Na hicho ndio alichomaanosha sema wengi wamekurupuka wakifikiri anaponda RR.Kukonda sijui, ila ni kawaida kwa matoleo ya zamani kuwa na muonekano mbovu tofauti na matoleo mapya.. we tafuta gari yoyote, anza kuicheki generations zake, kuanzia ya kwanza, ya pili, ya 3, ya 4 kama ipo utaona gen 1 tofauti sana na ya 4.
Mbona TATA haziko nzuri wala imara kama LR. Kumilikiwa na TATA haina maana imekuwa ya Kihindi. Katika mkataba wao hata production itabaki pale pale UK na vitu vingine vyote vitabaki kama LR ya miaka yote.Range ni muhindi piwa
🤣🤣Leo leo leoo kazi ipooKwa speicifaction na ufanisi bora Land cruiser LC300 ni bora kuliko aina yeyote ya range rover.
Umeeleza vizuri sanaInategemea na mtumiaji.. kusema aina yeyote ya RR si kweli, Range Rover hizi latest zina luxury features ambazo LC haina, mfano mdogo tu RR hizi latest ni all wheel steering , ukipiga kona na tairi za nyuma zinapiga kona...
wenyewe wanasema RR zina cutting edge luxury features..
Mfano SV autobiography ,Ukija kwenye mwendo, muonekano, nguvu, interior na luxury LC haifiki, LC itaizidi RR kwenye durability..
Kinachopelekea RR kutokuwa reliable ni jinsi ilivyo complex kwenye electronics na mechanical tokana na luxury features ilizonazo... mfano hio feature ya all wheel steering tayari inaongeza complexity , hivyo RR latest ikipiga kona ina turning circle ndogo, unaweza piga kona katikati ya barabara ya njia moja na kugeuka chap...
Land Rover wame focus zaidi kwenye innovation, luxury features kuliko durability...
Wateja wa RR wanaangalia status, luxury, capability n.k kuliko durability, wateja wa LC watafocus zaidi na reliability...
Kwanini kaka unasema kazi ipo!?🤣🤣Leo leo leoo kazi ipoo
Hapo kuhusu stability na comfort mzee umetupiga.Nadhani kukosekana kwa Highway Dar kumemfanya jamaa asijue speed ya Range.
Range inakupita road kama umesimama na wala haiyumbi, wakati LC Toyota ukiendesha over 160 mvua ikiwa inanyesha unatafuta kifo.
Hakumbuki kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na story kuwa hata haitakiwi kupita karibu na BoT.
Vilevile stability na comfort ya Range road unaweza kweli ukalinganisha na aina yeyote ya Toyota, Jamaa nadhani ameumua tu kuidhalilisha Range.
Mkuu maana ya RR kuwa luxury oriented ni pamoja na comfort, LC haiwezi kufikia comfort iliyopo kwenye RR, jaribu hata kufuatilia mitandaoni huko. RR autobiography mfano ulinganishe na comfort ya LC? upo serious?Hapo kuhusu stability na comfort mzee umetupiga.
Ichukue range ipeleke chaka halafu ichukue land cruiser iinhize chaka ipi itatikisika sana kuliko nyingine!?
Dah Mkuu! Nakupa taarifa tu LC haipo kwenye orodho ya gari zenye hadhi Duniani! Ni gari ya Africa na Asia. Kuna nchi unaweza kaa mwaka haujaiona barabarani. Hata Hapo bongo kuna baadhi ya wadau muhimu ugoma kuitumia kwa kigezo kuwa haina hadhi na siyo salama. Umewahi ona mara ngapi Range imepata ajari kwa kubinuka matairi juu! Lakini kuna mifano mingi (hata wewe unajua) ya LC kupinduka miguu juu katika maeneo ambayo hata siyo hatarishi kiivyo.Hapo kuhusu stability na comfort mzee umetupiga.
Ichukue range ipeleke chaka halafu ichukue land cruiser iinhize chaka ipi itatikisika sana kuliko nyingine!?
Mmmh mkuu hapa unanipiga kamba.Dah Mkuu! Nakupa taarifa tu LC haipo kwenye orodho ya gari zenye hadhi Duniani! Ni gari ya Africa na Asia. Kuna nchi unaweza kaa mwaka haujaiona barabarani. Hata Hapo bongo kuna baadhi ya wadau muhimu ugoma kuitumia kwa kigezo kuwa haina hadhi na siyo salama. Umewahi ona mara ngapi Range imepata ajari kwa kubinuka matairi juu! Lakini kuna mifano mingi (hata wewe unajua) ya LC kupinduka miguu juu katika maeneo ambayo hata siyo hatarishi kiivyo.
Kiongozi Range rover wanayo gari yao kwa ajili ya ulinzi , ambayo ni Range Rover sentinel, ndio hio umemuona Samia anapita nayo majuzi na kwenye huu uzi juu posts za mwanzoni kuna mdau ameweka picha yake...Mmmh mkuu hapa unanipiga kamba.
Unaizungumzia LC300 au Land cruiser kiujumla??
Kama unazungumzia Land cruiser kiujumla basi hakuna nchi isiyotumia Land cruiser. Tena Toyota hupokea special order za kuunda ARMORED landcruiser.
Kipindi Rishi Sunak ni waziri mkuu kwenye convoy yake armored Land cruiser VX zilikuwemo na huyo ni waziri wa Uingereza.
Serikali nyingi Asia,South America hata baadhi ya European nations wanatumia Land cruiser.
UN tizama maeneo yote ya hatari wanayoenda hukuti wakitumia gari zingine zaidi ya landcruiser.
Iwe nchi zozote zile duniani hukuti wakitumia gari tofauti na land cruiser. Kwahiyo wao UN hawajui gari reliable!?
Toyota huwa wanapokea special order ya kuzi PIMP land cruiser ziweje.
Land cruiser utayoitumia wewe sio sawa atayoitumia mtu wa Ulaya.
Kuna land cruiser ukizipiga RPG hazilipuki. Bongo unazipata!??
Hizo ndio unakuta zinaanzia $ 500,000.
Magaidi wote na waasi wote umewahi kuona wanatumia gari za vita tofauti na land cruiser pickup za engine ya 1hz?
Ifunge rocket launcher nyuma ya Range au land rover halafu ifyatue uone kama hatujaizika hiyo Rover yako.
Embu ichukue Range rover yako kaipigishe mbizi jangwani uone kama itatoboa kwenye mchanga wa jangwani.
LABDA KAMA UTASEMEA land cruiser LC300 peke yake.
Ila kama unazungumzia LAND CRUISER KIUJUMLA weeeh! Kafanye tafiti vizuri.
Hapo sijazungumzia LC300 peke yake. Bali nimezungumzia Land cruiser zote kiujumla hadi land cruiser pickup.Kiongozi Range rover wanayo gari yao kwa ajili ya ulinzi , ambayo ni Range Rover sentinel, ndio hio umemuona Samia anapita nayo majuzi na kwenye huu uzi juu posts za mwanzoni kuna mdau ameweka picha yake...
Sentinel zinakuwa kwa wingi kwenye misafara ya waziri mkuu wa Uingereza , ni heavily armored, luxury SUV ambayo inakuwa designed na Land Rover wenyewe kwa ajili ya ulinzi wa viongozi/watu mashuhuri n.k...
Land Cruiser ambayo ni armored haitengenezwi na Toyota wenyewe, kuna makampuni yanayohusika na kutengeneza (armoring companies), wanaiununua hio gari, wana i disassemble halafu wanaweka ballistic steel, armored glass, suspension, run flats n.k...
Na hizo gari huwa wanazi certify tokana na uwezo ilionao wa kuhimili milipuko, mashambulizi ya risasi n.k.. kwa kipimo wanaita VR, ambapo maxmum level ni VR10, hio sentinel ina VR8...
Kuna gari nyingi tu kutoka makampuni mengine ambazo ni armored na ni imara sana, mfano Audi 8L, hio anatumia hata waziri mkuu wa Uingereza, hivyo tusikariri tu Range Rover na Land Cruiser, hio A8L ni sedan lakini kwenye VR level ina VR9 huko Range rover ina VR8, Land cruiser mara nyingi zina VR7 hasa hizi wanatumia marais wa huku Africa...
Hio sentinel ina uwezo wa kuhimili bomu chini ya gari ama juu ya gari, ina emergency exit, ina uwezo wa kuzuia risasi kutoka kwenye AK47... na ni gari imetengenezwa ku escape mashambulizi which means ina mbio, hivyo inakimbia hata kama tairi zikipigwa zikawa flat....
Hivyo Range ROver hio sentinel ikitokea shambulizi, ina uwezo wa ku escape na kukimbia kutoka eneo la tukio kwa kasi kuliko hio LC 300 ambayo pia ni armored, kumbuka RR sentinel inatoka kiwandani ikiwa imetengenezwa na Land Rover wenyewe...
Hio LC 300 inakuwa modified na hizo kampuni za armoring, hivyo wanaiongezea uzito zaidi tofauti na toyota wenyewe walivyokadiria uzito wake na perfomance kutoka kiwandani...
Ndio maana katika hiki kipindi ambacho nchi yetu inapitia changamoto za kiusalama hasa kwa viongozi kamati ya ulinzi wa rais Tanzania wakaona wapendekeze hio Sentinel na kuiacha Land Cruiser....
Una moyo sana.Kiongozi Range rover wanayo gari yao kwa ajili ya ulinzi , ambayo ni Range Rover sentinel, ndio hio umemuona Samia anapita nayo majuzi na kwenye huu uzi juu posts za mwanzoni kuna mdau ameweka picha yake...
Sentinel zinakuwa kwa wingi kwenye misafara ya waziri mkuu wa Uingereza , ni heavily armored, luxury SUV ambayo inakuwa designed na Land Rover wenyewe kwa ajili ya ulinzi wa viongozi/watu mashuhuri n.k...
Land Cruiser ambayo ni armored haitengenezwi na Toyota wenyewe, kuna makampuni yanayohusika na kutengeneza (armoring companies), wanaiununua hio gari, wana i disassemble halafu wanaweka ballistic steel, armored glass, suspension, run flats n.k...
Na hizo gari huwa wanazi certify tokana na uwezo ilionao wa kuhimili milipuko, mashambulizi ya risasi n.k.. kwa kipimo wanaita VR, ambapo maxmum level ni VR10, hio sentinel ina VR8...
Kuna gari nyingi tu kutoka makampuni mengine ambazo ni armored na ni imara sana, mfano Audi 8L, hio anatumia hata waziri mkuu wa Uingereza, hivyo tusikariri tu Range Rover na Land Cruiser, hio A8L ni sedan lakini kwenye VR level ina VR9 huko Range rover ina VR8, Land cruiser mara nyingi zina VR7 hasa hizi wanatumia marais wa huku Africa...
Hio sentinel ina uwezo wa kuhimili bomu chini ya gari ama juu ya gari, ina emergency exit, ina uwezo wa kuzuia risasi kutoka kwenye AK47... na ni gari imetengenezwa ku escape mashambulizi which means ina mbio, hivyo inakimbia hata kama tairi zikipigwa zikawa flat....
Hivyo Range ROver hio sentinel ikitokea shambulizi, ina uwezo wa ku escape na kukimbia kutoka eneo la tukio kwa kasi kuliko hio LC 300 ambayo pia ni armored, kumbuka RR sentinel inatoka kiwandani ikiwa imetengenezwa na Land Rover wenyewe...
Hio LC 300 inakuwa modified na hizo kampuni za armoring, hivyo wanaiongezea uzito zaidi tofauti na toyota wenyewe walivyokadiria uzito wake na perfomance kutoka kiwandani...
Ndio maana katika hiki kipindi ambacho nchi yetu inapitia changamoto za kiusalama hasa kwa viongozi kamati ya ulinzi wa rais Tanzania wakaona wapendekeze hio Sentinel na kuiacha Land Cruiser....
Land cruiser hizo wanatumia vikundi vya kivita ni kwa ajili ya reliability, haihusiani na uwezo wa gari kuhimili mshtuko pale silaha inapopiga...Hapo sijazungumzia LC300 peke yake. Bali nimezungumzia Land cruiser zote kiujumla hadi land cruiser pickup.
Na ndio maana nikafafanua hadi uwezo wa land cruiser pickup kubeba mini-multi launcher rocket system nyuma yake.
Je kuna aina ya land rover inayoweza kufungwa MLRS ndogo na ikahimili launching force yake!??
Sio tu MLRS hata missile launcher hufungwa nyuma ya land cruiser pickup kitu ambacho sijawahi kukiona katika gari za Land rover.
-Toyota wanaunda pia armored vihecle bro directly kutoka katika kampuni yao kwa order.
Huwa nawafuatilia sana hawa jamaa.
Waarabu wengi hununua armored vehicle directly kutoka Toyota ila baada ya kuweka order kwamba bana niundieni hii gari kwa mtindo huu na huu.
Naeleza nachokijua kaka.
Ila kumbuka nimeeleza landcruiser kiujumla sio lc300 peke yake.
-Na nimemkatalia jamaa kusema kuwa "hukuti nchi nyingine cruiser zikitumika eti viongozi wa nje hawatumii" ilhali Rishi Sunak alitumia kwenye msafara wake cruiser VX.