Ramaphosa akabiliwa na tuhuma za ufisadi

Ramaphosa akabiliwa na tuhuma za ufisadi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Taasisi ya kupambana na rushwa nchini Afrika Kusini imesema rais Cyril Ramaphosa alilidanganya bunge kwa kukusudia kuhusu mchango wa kampeni.

Madai haya yanaonekana kuwa kizingiti kipya kwa rais Ramaphosa aliyeapa kupambana na ufisadi uliomlazimisha mtangulizi wake Jacob Zuma kujiuzulu na kuibua ghadhabu ya umma.

Ripoti ya mlinzi wa mali za umma iliyotolewa jana imesema Ramaphosa aliwandanganya wabunge kwa makusudi mwishoni mwa mwaka jana kuhusu mchango wa kampeni wa dola 34,000 uliotolewa na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Africa Global Operations awali ikijulikana kama Bosasa.

Ripoti hiyo inamtaka mkurugenzi wa mashitaka ya umma kuchunguza zaidi madai hayo.

Ofisi ya Ramaphosa imesema rais huyo hajafanya kosa lolote na kumtaka mlinzi wa mali ya umma kuanzisha uchunguzi dhidi yake.
 
Ofisi ndio inamtakasa si wasubiri uchunguzi wa DPP. Hawa marais wa kiswahili ni tabu sana. Sisi waafrika hatukupashwa kudai uhuru, ona sasa tunavyoumbuka. Bogus kabisa.
 
Back
Top Bottom