nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
JUMAPILI, MEI 05, 2013 06:03 NA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM
WAKATI baadhi ya wanasiasa wakubwa nchini wakitajwa kuanza maandalizi ya chini chini kujipanga kusaka ukuu wa dola mwaka 2015, Mwenyekiti wa Taasisi ya Haki za Binadamu na Maendeleo ya Kiuchumi ya Watu wenye Ulemavu, Abubakary Rakesh (53), amevunja ukimya na kusema kuwa atagombea nafasi ya urais endapo chama chake cha Alliance For Democratic Change (ADC) kitamteua.
Akizungumzana MTANZANIA Jumapili, Rakesh alisema dhamira hiyo imekuja baada ya kuona mambo mengi ndani ya nchi, hasa kwa watu wenye ulemavu hayaendi sawa na wawakilishi wa Bunge baadhi yao wamekuwa wakitumia ukumbi wa Bunge kama Uwanja wa kuchezea taarab.
Tangu mwaka 2005 niligombea ubunge katika Jimbo la Muheza mkoani Tanga ambapo niliambulia kura 7,000 na mgombea mwenzangu ambaye nilikuwa nikichuana naye alipata kura 54,000. hivyo nikalikosa jimbo, alisema Rakesh.
Alisema kutokana na matokeo hayo hakukata tamaa na alijaribu tena kugombea nafasi hiyo katika jimbo hilo mwaka 2010, ambapo kura hizo ziliongezeka na kufikia 11,000 na mbunge wa sasa, Herbert Mtangi alipata kura 35,000.
Rakesh aliongeza kuwa kwa sasa nia ya kugombea ubunge ameiondoa kabisa, kwani ameona bungeni si mahala pa heshima na hivyo kuamua kuusaka urais.
Alisema kama Rais Jakaya Kikwete ana eneo ambalo anatakiwa kulifanyia kazi na kulijengea nidhamu ni eneo hilo la Bunge.
Kwa kweli bunge letu la sasa ni aibu tupu, kwani kama kuna eneo ambalo Rais Kikwete ana kazi basi ni bungeni, hivyo mimi nimeona bora niingie kwenye kinyanganyiro cha urais, nina imani nitajijengea heshima kuliko kwenda kurushiana vijembe vya kwenye taarabu, alisema Rakesh.
Alisema ameshuhudia Bunge la nyakati hizo lililoongozwa na spika watatu tofauti, lakini hayakuwahi kutokea mambo kama yaliyopo hivi sasa, hivyo Rais Kikwete ana kazi kubwa ya kurekebisha changamoto hiyo ili kurudisha heshima ya Bunge hilo.
Alisema historia na dhamira ya kweli ya ushindi wa nafasi hiyo anauona upo wazi, kwani idadi ya wanachama wake ni Mil 4.8 na Rais Kikwete alipigiwa kura na kushinda na wananchi Mil. 4.
Hii idadi ya wanachama wangu tu inatosha kunipitisha mimi katika nafasi hii, kwa sasa nimeweka dhamira ya kweli na nina uhakika nitapita kwa kishindo na nitakuwa mwakilishi mzuri wa kundi hili ambalo limesahaulika, alisema Rakesh.
Aliongeza utafiti uliofanyika mwaka 2011 ulionesha kuwa asilimia 0.7 ya walemavu ndiyo wanaofanya kazi ya kuajiriwa Dar es Salaam kati ya wafanyakazi 600,000 walioajiriwa, hivyo akichukua nafasi hiyo atahakikisha usawa unapatikana kwa kuzingatia vigezo mbalimbali.