Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,815
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini tarehe 9 Machi 2016. Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza uhusiano baina ya Vietnam na Tanzania mbao umedumu kwa zaidi ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake pamoja Kufungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam.
Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo Barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka 2011, ambapo nchi nyingine anayotarajiwa kutembelea ni Mozambique. Rais Truong anatarajiwa kufuatana na mke wake Bi Mai Thi Hahn, mawaziri 4 wanaoshughulika na sekta za Kilimo, Mawasiliano Uwekezaji, Afya Viwanda na Biashara. Aidha mgeni huyo atafuatana na ujumbe wa wafanyabiashara 30 kutoka Vietnam.
Mahusiano ya Vietnam na Tanzania
Katika jitihada za kuimarisha mahusiano, mwaka 2001 Tanzania na Vietnam zilisaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kuichumi na ufundi. Mkataba huo uliainisha maeneo ya ushirikiano yafuatayo:
Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo Barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka 2011, ambapo nchi nyingine anayotarajiwa kutembelea ni Mozambique. Rais Truong anatarajiwa kufuatana na mke wake Bi Mai Thi Hahn, mawaziri 4 wanaoshughulika na sekta za Kilimo, Mawasiliano Uwekezaji, Afya Viwanda na Biashara. Aidha mgeni huyo atafuatana na ujumbe wa wafanyabiashara 30 kutoka Vietnam.
Shughuli za msingi zitakazofanyika kwenye ziara
- Wakati wa ziara hiyo Rais Truong Tang San atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar-es-Salaam.
- Aidha, Rais Truong pia atapata fursa ya kutembelea eneo la EPZ la Ubungo kuangalia viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za kuuza nje ya
- Baada ya kutembelea EPZA Rais Truong atahudhuria mkutano wa biashara na uwekezaji katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Vietnam.
- Rais Truong atamaliza ratiba yake kwa kuhudhuria dhifa ya Taifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.John Pombe Joseph Magufuli.
- Mahusiano ya Tanzania na Vietnam yaliyojengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi wa Vietnam Ho Chi Minh mwaka 1960 na kupelekea kuanzishwa rasmi kwa mahusiano ya kidiplomasia mwaka 1965. Kwa muda mrefu mahusiano hayo yalikuwa ya kisiasa zaidi ambapo Tanzania iliunga mkono harakati za Vietnam za kupinga uwepo wa majeshi ya kigeni kwenye ardhi yake.
Ziara za Kukuza Mahusiano za Viongozi Wakuu
- Aidha katika kipindi cha miaka 50 ya mahusiano ya kidiplomasia baina ya Vietnam na Tanzania, viongozi wa kitaifa wa nchi hizi mbili wamefanya ziara za kudumisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Tarehe 25 Septemba 1973, Rais wa Vietnam Mheshimiwa Nguyen Huu Tho alifanya ziara nchini Tanzania.
- Kwa upande wa Tanzania, viongozi waliofanya ziara nchini Vietnam ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa (2004); Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (2014), Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk Ali Mohamed Shein (2012); Mawaziri Wakuu wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Edward Lowassa (2006); na Mhe. Mizengo Kayanza Pinda (2010).
Mikataba ya Mahusiano baina ya Tanzania na Vietnam
Katika jitihada za kuimarisha mahusiano, mwaka 2001 Tanzania na Vietnam zilisaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kuichumi na ufundi. Mkataba huo uliainisha maeneo ya ushirikiano yafuatayo:
- Kubadilishana uzoefu katika sekta ya kilimo na maendeleo vijijini;
- Kubadilishana uzoefu katika matumizi ya sayansi na teknolojia katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, uvuvi na misitu;
- Kupeana taarifa za fursa za masoko ya bidhaa za kilimo
- Vietnam kuipata Tanzania utaalam na teknolojia ya uvunaji na utunzaji wa maji
- Mwaka 2014 Tanzania na Vietnam zilisaini Mkataba wa ushirikiano katika sekta ya mawasiliano ambapo kupitia mkataba huo kampuni ya Vietel inayomilikiwa na Jeshi la Vietnam imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya mawasiliano nchini na kuzalisha ajira za moja kwa moja kwa watanzania 1600 na fursa za kujiajiri kwa watanzania 20,000. Vilevile,kampuni hiyo kupitia mkataba uliosainiwa,itatoa huduma za internet bure kwenye mashule na mahospitali ya Serikali vijijini.
-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dar es Salaam
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dar es Salaam
03 Machi, 2016
HAPA KAZI TU!