Raisi wa JMT apunguziwe madaraka hasa ya kuteua viongozi.

kinepi_nepi

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
869
235
Natoa wito wa kumpunguzia Raisi wa JMT madaraka makubwa aliyonayo pamoja na kupunguziwa uwezo wa kuendelea kutaja majina kwa ajili ya kuteuwa viongozi na wakurugenzi mbali mbali. Vivile kuondoa wabunge kumi wanaoteuliwa na Raisi kwani hawana Tija.

Raisi akiachiwe wachache wa kuteua lazima waidhinishwe na bunge, na kuwe na njia za kuwatoa bila kumsubiria Raisi pale wanapochemsha kazi. Mawaziri wasiwe wabunge ili bunge liwe sehemu ya muhimili mmoja sio miwili.
 
Huo ni wito au mapendekezo yako katika mchakato wa kubadilisha katiba. Kama unamaanisha hivyo basi ni vizuri ukasubiri wakati ukifika uwasilishe maoni hayo kunakohusika. Kama unazungumzia kwa frame work ya sasa basi huo ni umbumbumbu kwa sababu katiba ya sasa inamruhusu Rais kufanya uteuzi anaoufanya na hilo halina matatizo ya kisheria na kimfumo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom