Raisi ajaye atoke wapi?

rsvp

JF-Expert Member
Dec 13, 2012
874
1,000
Kumekuwa na makundi na uashabiki wa kutaka Rais wa Tanzania atoke upande fulani au chama fulani.
Lakini,shida imekuwa na Viongozi wanaojali maslahi yao Binafsichi.

Sasa naomba tutafakari Rais ajaye ataweza kupatikana kutoka katika kundi gani la jamii:na akawa Rais bora wa kuongoza nchi.

[1].Tajiri sana,;inawezekana akawa hana tamaa ya mali kwa vile ni tajiri,lakini upande mwingine wa shilingi anaweza tumia madaraka kuendeleza,kujimbikizia ,na kulinda mali zake na mwisho wa siku kusahau maslahi ya wanyonge na nchi kwa ujumla.
[2].Middle class,;kupata kiongozi wa kutoka kundi hili inakuwa ni vigumu kwani wengi wanapenda kulinda heshima ya nafasi zao katika jamii ,na wengi katika kundi hili ni wafanyakazi,na watu wenye taalum zao na hwapendi siasa.
[3].wanasiasa;hawa wanafuata maslahi ya kundi fulani linalokuwa limemjenga na kumpa nadfasi ya uwakilishi,na mara nyingi hawajali maslahi ya Taifa.
[4]Mwananchi wa kawaida;kundi hili kupata nafasi za juu za uongozi ni ngumu ,kwani kundi hili halina fedha za kupenya katika nafasi za uongozi labda Mapinduzi au mazingira yenye FAIR PLAY

Sasa Angalia mifano wa Marais walioitawala Tanzania walikotokea:
[1]J.K.Nyerere alikuwa mfanyakazi pale PUGU,lakini akawa mkazi wa MAGOMENIi ,halafu apata Uwaziri Mkuu halafu Rais wa Tanzania.
[2].A.H.Mwinyi alikuwa mfanyakazi,halafu Balozi EGPTY,Waziri,lakini nasikia anafamilia pale TEMEKE,halafu RAIS wa Zanzibar na RAIS wa Tanzania.
[3]B.W.Mkapa,alikuwa mfanyakazi,halafu Waziri,mkazi wa UPANGA,na RAIS wa tatu wa Tanzania.
[4].J.K.Kikwete,aliungia siasa,baadae akawa anapatikana Kijiwe cha KARIAKOO na Pale MAGOMENI,akawa Waziri ametokea MIKOCHENI na hatimaye Rais wa nne wa Tanzania.

Inawezekana RAIS ajaye akatokea kwenye makazi yafuatayo:VINGUNGUTI,SINZA,TANDIKA,KIGAMBONI,MBAGALA,TEGETA,MWENGE,KAWE ,SEGEREA,TABATA,GONGO LA MBOTO?!!

JE?Elimu ya RAIS inaweza kusaidia?au ni utashi wa Kiongozi kwani Rais wa KWANZA alikuwa na MASTERS,Rais wa PILI nasikia alikuwa na DIPLOMA,Rais wa TATU alikuwa na MASTERS,na Rais wa Tatu ana Digrii moja japo anataka kuvunja rekodi kwani nasikia anaitwa Dkt japo Rais wa Amerca sijasikia kama wenye PHD wanapata nafasi ya kuwa Rais wa nchi.

Rais atakayepatikana 2015 atatokea makazi niliyoyaorodhesha hapo juu na hawezi kuhamia DODOMA.!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom