mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Mh.Magufuli katika kampeni zako uliahidi unataka kujenga Tanzania Mpya.Ni wazo zuri sana tumelikubali.Ombi letu kwako Kwa kuwa una uchungu Na nchi hii tunakuomba ufikirie jinsi Kodi za walala hoi wa Nchi hii zilivyotumika kuandaa Rasimu ya Katiba , Kurekebisha Jengo la bunge, Kuwalipa posho wajumbe 600 Na mwisho wa siku hakuna cha Katiba.Mh.Magufuli tunaitaka Rasimu ya Warioba kwani ndio maoni Yetu Na sio vinginevyo.Mh.Magufuli Haya majipu unayohangaika nayo in ubovu wa Katiba iliyopo.Mh.Magufuli tukamilishie
Katiba Yetu Kwa kuwaacha wanasiasa kando kwani wao ndio walioharibu Rasimu ya Warioba iliyokuwa Na Misingi mizuri.
Katiba Yetu Kwa kuwaacha wanasiasa kando kwani wao ndio walioharibu Rasimu ya Warioba iliyokuwa Na Misingi mizuri.