ABEL MAGEMBE LUGIMBA
Member
- May 22, 2016
- 63
- 59
RAIS WETU DKT MAGUFULI NI MKOMBOZI WA WANYONGE,WANAOMBEZA KWA KAZI NZURI ANAYOIFANYA WALAANIWE MILELE KATIKA JINA LA YESU KRISTO.
Niwajibu wetu Watanzania wazalendo wote kumuunga mkono Rais wetu Dkt Magufuli kwa kazi nzuri na ngumu anayoifanya ya kupambana na wahujumu uchumi . Amejitoa sadaka kwa ajiri yetu wananchi masikini ambao ni muda mrefu tulikuwa tunaonewa, tunanyanyaswa na kudhulumiwa haki zetu na watu wachache ambao waliifanya nchi yetu kuwa shamba la bibi. Rais wetu Mpendwa Dkt Magufuli amerudisha heshima yetu na utu wetu Watanzania.
Kila mmoja wetu katika Imani yake anatakiwa kuwa anamuombea Rais wetu kila Muda ili Mwenyezi Mungu amlinde sikuzote za maisha yake. Kwani ni ukweli usiopingika kwamba Mafisadi, majambazi, vibaka wote, watendaji wabovu wa serikali na wapiga dili wote wanamchukia sana Rais wetu.Sio muda wa kubeza na kumvunja moyo Rais wetu bali ni muda wa kumuunga mkono kwa kila jambo analolifanya kwa maslahi ya wananchi wanyonge wa Tanzania.
Tuwafichueni watu wote wanaoihujumu serikali ya Magufuli bila kuogopa vitisho vyao maana tupo katika Vita kali kati ya kundi kubwa la wajenga nchi yetu na kundi dogo la watu wanaoibomoa nchi yetu kwa kutuibia Raslimali zetu.Silaha ya kuishinda vita hii ni Kushikamana sisi wanyonge na kutengeneza umoja wenye nguvu,kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Mungu amlinde na kumbariki sana Rais wetu kwa kazi nzuri anayoifanya kwa ajiri ya sisi watanzania wanyonge.Na alaaniwe mtu yeyote anayemuombea mabaya Rais wetu Dkt Magufuli.