Rais wetu 2015+ ni huyu hapa!

Rais wetu 2015+ ni huyu hapa!

TECH WIZ

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2013
Posts
1,675
Reaction score
555
Rais tumtakae 2015 ni lazima:Awe mzalendo kwa vitendo;

Awe na uchungu na Rasilimali zetu;Achukie ufisadi na rushwa na lazima atuonyeshe kuwa anakerwa na mambo kwa dhati;Aheshimu Demokrasia;Asiwe mKabila,mDini au mKanda;Asiwe na kashfa za Ufisadi;Asiwe na tamaa ya madaraka;Asiwe ni miongoni mwa walio laaniwa na Baba wa Taifa;Awe ni mwanaSiasa anayependelea siasa safi;

Anayechukia na kuzikemea siasa chafu;Awe ni mwenye maono ya mbali;Mwenye mawazo ambayo yalileta matokeo mazuri iwe katika Chama chake cha Siasa au serikali aliyowahi kuitumikia;Awe anapendelea uwazi na awe tayari kutuambia Watanzania kiasi cha mali anachomiliki na atuambie namna alivyoipata hiyo mali;

Aiunge mkono Rasimu ya Katiba mpya;Akerwe na matumizi makubwa yasiyo na tija kwa Taifa yanayofanywa na Serikali;Achukie uchumi unaendeshwa kwa Mikopo;Akerwe na deni la Taifa;Achukie mfumko wa Bei;Achukie uduni wa miundo mbinu yetu ya barabara na reli;Na awe anapendelea diplomasia ya kiuchumi na Mataifa mengine.

Huyo ndiye hasa Rais tumtakae 2015.
 
Asijihusishe na madawa ya kulevya wala kuwachekea wanaofanya biashara hiii
 
Umetaja mengi sana
Hivi mkuu unadhani hapa duniani kuna binadamu ambaye yuko perfect?

Huwezi kuwa na yote hayo uliyotaja hata tukikuchagua wewe lazima utakuwa na dosari zako, uwe CCM au Chadema wote ni binadamu tu
 
Napita njia tu

Inamaana hakutakuwa na raisi mpya 2015?

Kwani mtu mumtafutae hayupo tz,
 
Simaanishi ni lazima awe na sifa zote hizo hapana lakini asipungukiwe na angalau sifa nne tena zilizo muhimu zaidi,Bin Fazza.Kutokuwa na kashfa ya UFISADI ni sifa muhimu zaidi.Nyingine zitafuata.
 
Hata hivyo hizo ndio sifa anazopaswa Rais ajaye awe nazo vinginevyo TANZANIA tutabakia kuwa shamba la bibi.
 
Umetaja mengi sana
Hivi mkuu unadhani hapa duniani kuna binadamu ambaye yuko perfect?

Huwezi kuwa na yote hayo uliyotaja hata tukikuchagua wewe lazima utakuwa na dosari zako, uwe CCM au Chadema wote ni binadamu tu
Lakini siyo ya kuuza madwa ya kulevya..
 
Hapana .mm nashauri kusiwe na uchaguzi 2015 kikwete aongezeww muda tu nchi itakuwa km africa kusini ,madini yatachimbwa,uranium,gesi,mabasi ya kasi,barabara za juu,daraja la kigamboni ,barabar vijijini kote,kuuza umeme hadi nje ya nchi,mji mpya wa kigamboni,kufufua viwanda nchi nzima japo ni mchina,kuindoa migogoro ya zanzibar,katiba mpya,ongezeni mengine wadau
 
sifa hizi ulizotaja mbona ccm hazipo kwa wanaotajwa kuwa ndo wagombea wao na haswa mtoa mapesa mengi nyumba za ibada?
 
Back
Top Bottom