Rais, Waziri TAMISEMI mulika mkoa wa Manyara

Rais, Waziri TAMISEMI mulika mkoa wa Manyara

scolastika

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
3,863
Reaction score
5,732
kwanza tuelewane sipo hapa kisiasa nipo hapa kuongelea uhalisia ndo maana sijapeleka uzi wangu jukwaa la siasa

Mheshimiwa Rais nikupongeze kwa kazi kubwa unayoifanya na pia kutengua uteuzi wa wateule wako pale usipordhishwa na utendaji kazi wao.

Mheshimiwa Rais pamoja na kazi kubwa unayoifanya ila umemsahau huyu mtoto wa nyerere huyu Makongoro kabla sijauzungumzia mkoa aliopo ningekuomba watu kama hawa watafutieni kazi zingine huko ambazo hazitaathiri watu moja kwa moja, Mwalimu Nyerere kuongoza vyema haimaanishi watoto wake nao wataongoza kama yeye mnawabeba sana ila ndo hivyo.

Kama nilivyoshauri hapo juu kama mnawabeba kwa title ya baba yao basi wataftieni vitengo huko,ila huku ambapo utendaji kazi wao una direct impact tuondoleeni

Malalamiko yangu kuhusu mkoa wa Manyara yanaenda kwa RC,RAS na viongozi wengine wa mkoa
Malalamiko yangu yatajikita kwenye Ofisi za umma mkoa wa manyara ,kwenye Elimu na Afya.
1.Ofisi za umma

kiufupi kwenye ofisi hizi utendaji wa kazi ni mbovu,especially halmashauri hali ni mbaya,watu wanafanya kazi kwa kurelax yaani hamna anayejigusa,ukisikia mtu anakwambia sijigusi bila shaka unaelewa

yaani mfano tuseme afisa utumishi maana yake yeye ata kazi ya siku moja anaweza akaifanya siku tano na wala hana wasiwasi , otherwise utangulize pesa,kuna NHIF nao ni shida yaani kadi wanaweza tumia hata miezi mitano kuitengeneza

Sina hakika kama kuna ufatiliaji kwenye utendaji kazi wao

2. Elimu
Ukitaka kustaajabu ya mkoa huu njoo ujionee mwenyewe kwa taarifa zilizopo yaliyotokea mwaka huu ndo yaliyotokea mwaka jana,iko hivi mkoa kama mkoa hawakuwa na habari zozote kuhusu mitihani ya mock kwa form four na form two,wakati mikoa mingine ikiendelea na mock basi wao wakasema itakuaje mkoa wetu hatujafanya mock form four? itaonekana ni wazembe basi hilo wazo likaja usiku tuseme jumanne tarehe 11 tarehe 12 wakawaita afisa elimu wilaya wote wakapewa hiyo amri, tarehe 13 wakuu washule wakapewa hizo habari njema wakaambiwa ratiba inawafata nyuma, kweli usiku ratiba ikawafata kwa mitihani ya prac na checklist ikatumwa.

yaani ratiba ibandikwe ijumaa halafu mtihani ufanyike Jumatatu na baada ya mtihani Mwalimu asahihishe makaratasi yake baada ya siku tatu afisa elimu mkoa anataka matokeo yake

Ebu tujiulize mtihani wa hivyo unalenga kumpima nini mwanafunzi anayejiandaa kufanya mtihani wa taifa?Je walikuwa wanawaza nini mpaka kuja kukurupuka mwishoni?

Ombi langu kwa Rais, waziri wa tamisemi na waziri wa elimu emu uangalieni vizuri huu mkoa ikiwezekana reform upya uongozi hii kitu sio mara ya kwanza

Afya leo ngoja niwaache kidogo,ila tabia za madaktari kulewa kupitiliza afu unaenda kuwahudumia wagonjwa kwenye medical ethics hicho kitu hakipo,na pia kuna madaktari hufanya operation kwa wajawazito wakati wa kujifungua hata ambapo hakuna ulazima huo ili mradi kuna hela ya operation(najua nnachokiongea)
 

MKUU WA MKOA WA MANYARA NI HEWA,SAMIA HAKUMUONA JUZI​

inawezekana wanamjua sema heshima ya baba wa taifa ndo shida inakoanzia mi nimeshauri apangiwe kazi zingine ambazo haxitagusa maslahi ya taifa moja kwa moja
 

Attachments

  • Screenshot_20220730-172556.png
    Screenshot_20220730-172556.png
    204.9 KB · Views: 10
Back
Top Bottom