Rais wangu Samia, soma hapa

Samia anayo kazi ngumu kushindana na propaganda alizosambaza hayati. I hope effect za kupeleka hela mtaani zitakuwa kubwa kwa siku za karibuni na kumlinda.

Wananchi wengi ni weupe kichwani, hasa wale masikini, walimwamini sana hayati kwa kauli zake za udanganyifu na ulaghai. Hili ongezeko la bei lawama zote anabeba Samia huko mtaani.

Hata hivyo mimi bado ninaona ccm waliweka watu wabovu kwenye nafasi ya uraisi na umakamu mwaka 2015.
 
Umenena vyema ila kuna watu chawa hawamwambii mama ukweli.

Ningekuwa rais ningekutafuta uwe chawa wangu maana wewe siyo mnafiki.
Wataniua
Bora nibaki huku huku kusikojulikana lakini niseme ukweli


I feel safe in JF kusema chochote kwa manufaa ya nchi yangu. Rais akiharibikiwa ni tumeharibikiwa sote
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Rais Samia ameituliza nchi, tumekuwa tukiishi kwa amani tofauti na yule SHETANI ambaye yeye mwenyewe alikuwa na vikosi vya kuteka, kutesa na kuua vikiendeshwa na akina Makonda na Sabaya.

Baadhi ya mambo mema aliyotutendea Samia ni kama:
- Watoto waliopata mimba wanarudi shule kusoma
-Madarasa zaidi ya 10,000 na vituo vya Afya vimejengwa nchi nzima
-Watumishi wa Serikali wameongezewa mishahara na posho
-Magazeti yaliyofungiwa yameachiwa kama Tanzania Daima
  • Waliobambikizwa makesi ya uwongo wameachiwa
  • Diplomasia ya kimataifa imefunguliwa na wawekezaji wanakuja nchini
-Kikosi cha kunyang'anya fedha za wafanyabiashara cha TRA kimevunjwa

Binafsi hata kama hamumpendi Samia lakini anafanya mambo yanayojenga uchumi wa nchi. Uwepo wake ni mpango wa Mungu
 
Ndugu yetu huyu katika imani
 
Umesahau na mfumuko wa bei
 
Hapa ktk nafasi ya waziri mkuu mnisaidiye nielewe.Kwa uelewa wangu hata kama waziri mkuu anamkubali au anakubalika si alitakiwa ajihudhuru uwaziri mkuu halafu wabunge wapige kura tena?Sasa hii kunga ndiyo sahihi?
 
Hapa ktk nafasi ya waziri mkuu mnisaidiye nielewe.Kwa uelewa wangu hata kama waziri mkuu anamkubali au anakubalika si alitakiwa ajihudhuru uwaziri mkuu halafu wabunge wapige kura tena?Sasa hii kunga ndiyo sahihi?
Nenda shule kajifunze kuandika ndio urudi hapa kutoa yaliyo moyoni kwako.
 
Mimi nimezungumzia udhaifu wa aina ya wagombea ccm iliweka.
Fine. Kama ccm iliweka wagombea dhaifu, ilibidi tuangalie walio bora huko kwingine tuwachague.

Walikuwepo wagombea bora kuliko wale wa ccm?!

That's my question.
 
Tuache unafki huyu mama Ana kura yangu 2025 no matter what , hayo mengine ongeeni tu ila kura yangu ni yake .

Nikikumbuka mateso tuliyopitia toka 2015 had 2021 hasa kwasisi watumishi wa umma nachelea kusema acha niwe mjinga kwa kumpa kura yangu huyu mama 2025.
 
Fine. Kama ccm iliweka wagombea dhaifu, ilibidi tuangalie walio bora huko kwingine tuwachague.

Walikuwepo wagombea bora kuliko wale wa ccm?!

That's my question.
Mimi sina jibu la swali lako.

Ccm wanapaswa kupitisha wagombea waliochunguzwa na kupimwa kwa muda mrefu.
 
Umekosea kumwambia kuwa ni yeye mwenyewe ndiye kiongozi wa mashambulizi kwa mtangulizi. Kwa mfano, alipoenda marekani na juzi Ghana, ametoa kauli zinazoonesha wazi kuwa yeye ni bora kuliko mtangulizi wake. Pia, kwa kauli zake anazojinasibu nazo ni kuwa sisi watanzania pamoja na chama chake bado hatuna imani naye kwa sababu ya jinsia yake.
 
Acha kelele tunaomkubali tupo wengi tu yaan subiri huo uchaguzi ufike Sasa hivi pambana na Hali yako,
Kwan wakati wa jiwe vyuma havikukaza?
Hata kipindi Cha mwendazake mlimpa matumaini. Ilipofika uchaguzi kwenye mikutano kila akienda wanaohudhuria ni wanafunzi kwa ajili ya mziki.

Mwishowe mkaenda kumficha Dodoma. Yetu macho ndugu.

Ila mngefanya mpango katiba mpya ikapatikana mambo yangependeza zaidi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…