Mheshimiwa rais wangu nimekuwa nikifuatilia kwa makini staili yako ya uongozi pamoja na hotuba zako nikagundua kuna kitu kimekosekana. Huenda huna washauri wazuri ama hufuati ushauri wao.
Kwa mfano Mheshimiwa namna ulivyoshughulika na sakata la sukari ni dhahiri ulihitaji ushauri wa wachumi. Hotuba yako ya UDSM imekupunguzia sana mvuto wako kwa wananchi walio wengi kwani lugha uliyotumia haiendani na haiba ya urais wa nchi.
Lugha kama "kamateni magari mtoe matairi muuze", .... "watoto wa UDOM ni vilaza"... "mzee kikwete umeaniachia kazi ngumu kila kitu hewa" n.k.
Pia kuna hoja za msingi unakwepa kuzitolea ufafanuzi kwa mfano ishu ya Lugumi, utekelezaji wa maazimio ya bunge juu ya escrow, Richmond, nk.
Nitaongezea baadae ngoja niingie ofisini kwanza.
NAENDELEA...
Kuna watu wananishambulia mimi badala ya kujibu hoja. Hawa bila shaka ni vijana wa Lumumba tuwapuuze....
Rais wangu mpendwa unahitaji kufuata ushauri. Kwa staili unayoenda nayo utachoka sana ifikapo 2020 hutatamani kugombea tena. Kwa kuwa umejitwisha baraza lote la mawaziri kichwani peke yako. Nchi kijiografia ni kubwa sana lakini unaendesha nchi kana kwamba tanzania ni DSM tu. Badala ya kujenga barabara za kupitisha mazao ya wakulima unajenga barabara ya kwenda kwenye upako! Nchi hii haihitaji upako inahitaji ibada ya kweli ambayo Mungu anaikubali.
Unamtetea VC wa UDOM eti kwamba asingekubali kuchukua wanafunzi "vilaza" angefukuzwa kazi, je, mbona akina marehemu Kabwe hawakupewa nafasi ya kujitetea? pengine nao walifanya hayo mnayodai walifanya kwa mashinikizo kama ambavyo alifanya Prof. Kikula.....