G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,766
- 36,626
Kweli rais wangu bado unaamini kuwa wewe ni kiongozi makini? Mimi siamini hivyo na kwa kweli hata kiwango kidogo cha umakini nilichokitarajia kutoka kwako siamini kama imekuwa hivi. Nahisi kama naota ndoto.
Sasa rais wangu, juzi ulifanya uteuzi wa wabunge sita wa kiume kinyume cha katiba ambayo inasema kuwa katika uteuzi wa wabunge 10 utakaofanya basi angalau watano wawe wanawake. Wewe tayari ukawa umeshavuka idadi ya wabunge wanaume ambao wanatakiwa wawe watano au chini ya hapo!
Sasa rais wangu, ukamteua Abdallah Possi kuwa balozi. Papo hapo akajiuzulu ubunge. Unadhani kuwa ubunge wake ulifutika? Kirahisi namna hiyo? Laah hasha! Ubunge wake bado uko palepale na atabaki kwenye k umbukumbu za bunge kama mbunge aliyewahi kuwa ndani ya jengo la bunge kama "Mbunge wa kuteuliwa na rais" Pia atalipwa mafao kwa muda aliotumikia na alilipwa mshahara wa bunge na alipewa huduma zote anazostahili mbunge! Hujaufuta kamwe ubunge wake.
Kwa rais makini kwa kitendo ulichofanya cha kuivunja katiba halali uliyoapa kuilinda, ulistahili kujiuzulu kwani wewe siyo kiongozi makini! Huzingatii katiba na wala huna muda nayo.
Natoa wito kwa bunge la Tanzania kuwa, Abdallah Bulembo na Palamagamba Kabudi wakishakula kiapo ndani ya bunge, basi wabunge waanze mchakato wa kumvua rais madaraka yake kwa kukiuka na kuivunja katiba ya nchi aliyoapa kuilinda kama jinsi ambavyo katiba hiyohiyo inavyolielekeza bunge pale ambapo rais ameenda kinyume nayo.
Hiyo siyo dhambi wala uchochezi bali ni kwa mujibu wa katiba yetu ya Tanzania!