Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Niliandika jana kuwa kuna wakati tunakuwa na viongozi njiti nikitaka ieleweke kuwa kuna viongozi wanakuwa katika vitengo fulani wakati haikuwa wakati wao! . Namna wanavyoishi ndio kitu kinachotupa ufahamu wa hivi Hasa kutokuwa na uwezo wa kuvumilia maneno ya nje..
Leo nitamfananisha rais wangu mpendwa na muwa mteta.
*Muwa mteta huwa una maji mengi lakini sio matamu.
*Huwa ni rahisi kuukata.
*Ukiwa wautafuna hutoa sauti kubwa kuliko uliokomaa
*hupenda kuzukukwa na majani au maganda mengi. Huohuo ukikomaa hufaa sana!!.
Rais wangu kipenzi umekuwa ukitoa kauli za kutushangaza, inaonesha muda mwingi unalala, unaamka unawaza uchaguzi wa 2020. Kauli zako zinakuchongelea hivyo kwetu.
Mpendwa Rais wangu umekuwa muda mwingi ukiotoa kauli ambazo zimenifanya nikuone kama awali hukujua kama ingewezekana wewe kuwa rais, na ilipotokea kama hukuamini vile........ , na ndio maana ulikuwa unaweza kuwa unatoa matamko ya kutoa hela kwenye idara fulani kwa mfano mahakama mwaka jana, hata ukiwa jukwaani na ukisema "hii ndio raha ya urais" sijui ulitaka nani ajue kama kuwa rais ni raha au laa.
Naskia hupendi kukosolewa , lakini mimi siamini kama kweli uko hivyo.
Mpendwa rais maamuzi yako mengi yameniaminisha kuwa umeupenda urais kuliko kawaida na hata kuiona miaka 5 kama ni kidogo sana hivyo unajitahidi kutumia na kuweka mazingira yatakayo kufanya ushinde tena 2020.
Kauli kama hizi.
"Mkurugenzi tunakupa gari, ulinzi, posho na nyumba, na bado unatangaza mpinzani ameshinda, hivi mna akili gani ninyi?...".
Mheshimiwa rais kauli hii inanifanya nikuone bado hujakomaa kidemokrasia na hauheshimu mawazo ya wananchi,RAIS HUWEZI KUSIFIWA NA KILA MTU,
Anaeamua nani aongoze ni wananchi sio wakurugenzi..
Kauli hii matokeo yake kama kweli wakurugenzi watafanya unavyotaka ni fujo na vurugu.
Hivi unajua kama wewe ni rais wa watanzania bila kujali vyama vyao? Unajua kuwa hizo posho unazowalipa hao wakurugenzi sio zako bali hao wapiga kura?.... Lakini unajua kama wapo wapinzani waliokupigia kura?, na wapo CCM WALIPIGIA KURA wapinzani?..... fikiria sana kabla ya kuchukua hatua yoyote mkuu
Lakini pia mheshimiwa rais, Juzi nilikuskia unasema mbunge yeyote wa ccm alietaka au alieenda kumtembelea Lema gerezani ni msaliti, hivi kweli ulimaanisha au ulikuwa unatania mkuu? Wewe ndiyo raia namba moja unaetakiwa kuhubiri amani, upendo na umoja hapa ulitufundisha nini mkuu?, hauamini maisha nje ya siasa?
Sisi wengine hatuipendi siasa kwa sababu tunaamini ni chanzo cha uovu, usipojirekebisha kwa kauli hizi na nyingine nyingi unatupa hofu kubwa mkuu. Naogopa kusema mengi lakini kwa sababu nakupenda acha nikuambie!!..
Mimi naamini kitendo cha wewe kuwa rais UNA NAFASI KUBWA SANA YA KUWAJIBU WAPINZANI WAKO KWA VITENDO NA SIO MANENO. WANACHI TUNAONA HATA WAKISEMA HAUTUFAI WAKATI TUNAKUONA SISI HATUWEZI KUWAPA KURA WAO TUKAKUACHA WEWE, lakini ukiwa unaongea kauli zinazoashiria kulipasua taifa hakika waamuzi ni sisi hapo 2020.
Nakutakia kazi njema... Ukiniona mchochezi sawa lakini nimeona niongee nilichojaliwa!....
NB:
Kukufananisha na muwa sijakufanya uwe muwa!.