Rais wangu kikwete sikia ushauri huu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wangu kikwete sikia ushauri huu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nkisumuno, Sep 18, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Chonde chonde Rais Kikwete watanzania tunakuangalia, dunia inakuangalia kuhusiana na matukio yanayoashiria uvunjivu wa amani ya Tanzania tuliyoizoea. Polisi wamegeuka chinja chinja rais umenyamaza kimya kama hakuna linalotokea, angalia yaliyotokea Arusha, songea, morogoro na juzi juzi mwandishi wa habari pale Nyololo Iringa. Kuna tetesi kuwa wewe na chama chako cha CCM ndiyo mnaowatuma polisi ili wapunguze nguvu ya CHADEMA, binafsi imenichukua muda mrefu kuamini lakini sasa nimeanza kuamini

  Kinachofanya niamini ni mazingira yenyewe kama vile ukimya wako, hakuna hata polisi aliyekamatwa, hata huyo aliyefikishwa mahakamani Iinga juzijuzi kafichwa sura, Kamhanda aliyeamuru Mwangosi auawe kuna tetesi mnataka kumhamishia makao makuu kwa nini tusianze kuamini hizo tetesi?

  Hakuna hata binadamu aliyepewa mamlaka ya kuua na ndiyo maana hata Mungu hakumpa uwezo mwanadamu kuumba.Fikiri juu ya hili ungekuwa wewe ndo unaguswa na matukio haya ungenyamaza kwa utashi tu wa siasa, ungekuwa wewe ndo Mwangosi kuacha watoto wadogo vile. Naomba toa karipio kwa jeshi la polisi waacche kuua raia vinginevyo Mungu ataingilia kati kutokana na manung'uniko ya Taifa hili hata wewe hutakuwa salama. Damu isiyo na hatia haipaswi kumwagika bure si kitu cha kawida kwenye Taifa ambalo wote tuliitana ndugu.

  Mwisho nitoe ombi la pekee; hata baada ya uchaguzi mkuu ujao naomba chonde kama Chadema watashinda wape haki yao vinginevyo itakuwa shida kwani hali iko waazi na hatuhitaji mtabiri kutuambia kilicho mbele yetu. Kemea jeshi lako na hata mawaziri wanaojipendekeza kwako hata kwa kusababisha migogoro. Nahitimisha kwa kusema madaraka uliyo nayo ni makubwa mno toa amri gazeti la Mwanahalisi pia lifunguliwe. Unapokuwa na vyombo vinavyokosoa kwa undani ni rahisi kujirekebisha. Sawa na mtu anayekuambia toa tongotongo jichoni anakupenda kuliko yule anayesema umependeza lakini kifungo umefunga vibaya. usipuuze ushauri huu unaweza kuliponya Taifa hili.

  Fikiri tangu Polisi walipoanza kuua raia je raia wanaogopa au ndo wanasonga mbele. Mabadiliko yanapokuja huja na hakuna anayeweza kuyabadilisha kwa njia yoyote ile kumbuka ta Libya na Tunisia
   
 2. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,969
  Likes Received: 6,744
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kutoa ushauri mzuri sana kwa Rais wetu, sidhani kama atakusikiliza, kwa kuwa kwa jinsi tukio la kuuawa Mwangosi lilivyotokea, ni wazi sasa inajulikana aliuawa na polisi, kwa maelekezo maalum, toka kwa RPC Kamuhanda,ambaye ndiye aliyeongoza operesheni hiyo. Kwa nchi yenye utawala bora kamili, ni lazima kesho yake tungesikia moja kati ya mawili, aidha Kamuhanda angeandika barua ya kujiuzuru wadhifa wake, na kama asingefanya hivyo, Rais aliyemteua kwenye nafasi hiyo, angemfukuza kazi mara moja. Kwa kuwa yote hayo hayajafanyika, tunapata uhakika usio na shaka yoyote kuwa mauaji ya Mwangosi yalikuwa na baraka zote, toka kwa mkuu wa nchi. Kwa hiyo ushauri huo, naweza kuufananisha na kumpigia mbuzi gitaa, hatakuelewa,badala yake, atakuangalia tu na kukushangaa!!
   
 3. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,122
  Likes Received: 1,209
  Trophy Points: 280
  Watu wote duniani wanaona haya. Kikwete is simply useless. Leo hii nilikuwa pale mambo ya nchi za nje kumuaga ndugu yangu anayekwenda tour hivi karibuni, yaani nilishangaa kusikia wafanyakazi pale wizarani wakimcheka Kikwete waziwazi. Wengine wanamuita msanii tena bila woga, nilisikia jokes pale za Kikwete haki ya Mungu sikuwahi sikia shemu yeyote ile hapa Dar. Huyu mtu hakufaa kabisa kuwa rais wetu, huyu ilibidi awe diwani tu au Mweneyeketi wa mtaa fulani lakini si rais.
   
 4. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,969
  Likes Received: 6,744
  Trophy Points: 280
  Jambo lingine la kutafakari, huyo huyo Kamuhanda alishasababisha mauaji mengine ya raia wasio na hatia huko Songea, badala ya kuchukuliwa hatua akapewa uhamisho wa kwenda Iringa ili akaendeleze mauaji mengine, hayo aliyomfanyia Mwangosi. Lakini Kamuhanda atambue damu ya Mwangosi na hao raia wengine, aloiwaua Songea haitapotea bure, ingawa kwa sasa anapata kinga kutoka kwa watawala, lakini atambue hakuna utawala wa hapa duniani uliowahi kudumu milele, hivi sasa atapiga chenga, lakini, Mungu muweza wa yote, kama alivyowaumbua wauaji, kwa zile picha zilizopigwa kule Nyololo, katika siku tusioijua sisi binadamu, mauaji haya lazima utayajibu, kama siyo katika mahakama za hapa TZ, basi utaburuzwa the Hague, pamoja na genge lako lote la akina JK, Mwema, Chagonja, Shilogile na wauaji wengine!!
   
 5. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nashukuru ndugu yangu tusichoke kumwambia ili siku yatakapompata mabaya akumbuke kuwa tulimwambia, na ndipo atakapokumbuka kuwa kina nape walikuwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Mwalimu wangu mmoja wa chuo aliwahi kuonya kuwa watu wengi hufa kwa kupuuza ushauri bora kwa ufupi alisema " Hufa wameambiwa".
   
Loading...